Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group muda mfupi
baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika shamba la Baba Wa Taifa
kijijini Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL
Group wakishiriki kupanda miti katika shamba la Baba wa Taifa,Mwalimu
Nyerere katika Kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakifanya usafi katika kata ya Ilomba eneo la Stendi ya Mabasi Jijini Mbeya katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
Baadhi
ya wafanyakazi wa TBL Mbeya katika picha ya pamoja baada ya kushiriki
kazi za usafi katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
………………………………………………………
–Wafanyakazi washiriki kuadhimisha Siku ya Mazingira
Katika
kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani 2017 Kampuni ya TBL Group iliyopo
chini ya kampuni ya kimataifa ya vinywaji ya ABInBev imetekeleza kwa
vitendo kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani nchini ya “Hifadhi
mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda, ambapo wafanyakazi wake
wameshiriki katika shughuli mbalimbali za maadhimisho.
Wafanyakazi kutoka viwanda vya TBL Group vilivyopo katika mikoa ya Dar
es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Moshi wameshiriki katika shughuli
za usafi wa mazingira na upandaji wa miti ambapo baadhi yao wameshiriki
katika maadhimisho ya kitaifa kijijini Butiama na kushiriki kampeni ya
kupanda miti iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni wa heshima.
Akiongea
kuhusu mkakati wa kampuni kuhusiana na suala ya mazingira, Afisa wa
Masuala Endelevu wa TBL Group, Irene Mutiganzi,alisema mazingira ni
suala ambalo kampuni inalipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa katika moja ya
malengo ya kampuni mama ya TBL Group ya ABiNBEV inayojulikana kama
‘Kujenga Mazingira ya Kuishi katika Dunia iliyo safi’ suala la utunzaji
mazingira linatekelezwa kwa vitendo katika maeneo yote ya biashara za kampuni.
Alisema
kwa kufuata mwongozo huu kampuni imejiwekea malengo ya kufanikisha
kuhusiana na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya matumizi mazuri ya
maji katika mchakato wa uzalishaji, kutumia nishati mbadala zisizochafua
hewa, kushiriki kampeni za kupanda miti na utunzaji wa vyanzo vya
maji,kutumia vifungashio rafiki kwa mazingira.
Kuhusiana na matumizi ya maji kwa umakini amesema TBL imepunguza matumizi ya maji katika mchakato wa uzalishaji wa bia kutoka
hectolita 6 za maji zilizokua zinatumika katika miaka ya karibuni hadi
hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa kwa sasa na
inaendeleza mkakati wa kupunguza matumizi zaidi ambapo pia imekuwa
ikifanya utakatishaji wa maji taka na kuharibu taka ngumu na nyepesi kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.
Mutiganzi
alibainisha kuwa kampuni tayari imeanza kutekeleza hatua za kufanya
uzalishaji kwa kutumia nishati mbadala zisizokuwa na athari kwa uchaguzi
wa hewa ambapo katika kiwanda cha TBL Mwanza kinafanya uzalishaji kwa
kutumia mashine zinazozalisha nishati zinazotokana na pumba za mpunga na
katika kiwanda cha TBL Mbeya zimefungwa paneli za umeme wa jua ambayo
inawezesha kupatikana umeme wa jua unaotumika katika baadhi ya shughuli
za mchakato wa uzalishaji.
Mutiganzi
alisema TBL Group inaliangalia suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo
vya maji sio kwa kiwango cha maslahi ya viwanda vyake kupata malighafi
tu bali kwa jamii nzima ambapo kampuni inafanyia biashara kwa kuwa sera ya kujenga ‘Dunia Maridhawa’ (Better World) inashahabiana Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) na suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni moja ya suala ambalo limepewa umuhimu mkubwa.
“Kupitia
sera ya kampuni ya ‘Kujenga Dunia Maridhawa’ tumeweza kutekeleza kwa
vitendo kanuni za utunzaji wa mazingira, Kuhamasisha jamii unywaji wa
kistaarabu na kuunga mkono jitihada za serikali kusaidia kufanikisha
changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii hususani katika sekta ya
afya,usalama barabarani na elimu na siku zote kampuni na wafanyakazi
wote tutaendelea kufanikisha uwekezaji wenye kuleta manufaa kwa jamii nzima”.Alisema Mutiganzi.
Sera
ya kujenga Dunia Maridhawa ya ABInBev ambayo inatekelezwa katika maeneo
yake yote ya biashara imejikita katika ufanikishaji wa malengo makuu
matatu ambayo ni ‘Dunia inayokua ‘ inayolenga kukuza shughuli mbalimbali
na kuwapatia watu fursa ya kujiendeleza kimaisha,’Kujenga Dunia iliyo
safi inayolenga kulinda mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo na
‘Kujenga Dunia ya watu wenye Afya ambayo inahimiza utumiaji wa vinywaji kistaarabu bila kuleta athari kwa jamii.
EmoticonEmoticon