WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 “KULAMBA” SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO

June 04, 2017
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, aliongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Neema Muro na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo, baada ya kufungwa kwa semina kwa wastaafu watarajiwa wa wilaya zote za mkoa wa Mwanza iliyofanyika ukumbi wa chuo cha watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, huko Capri-point jijini Mwanza.
Katika hotuba yake aliyotoa Kati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw. Mayingu alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi Trilioni 1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18.
 
”Kwa mwaka 2017/18 pekee, Mfuko unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia shilinginTrilioni 1.3.Kisai hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia semina hii Wastaafu watarajiwa wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga
maisha yao baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji wa mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na kuongeza fursa za ajira.” Alisema Bw. Mayingu katika hotuba yake.
 
 Miongozi mwa mambo waliojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika 450, ni pamoja na uanzoshwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinumbalimbali za ujasiriamali. 
 
Bw. Kuhusu mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw. Mayingu alisema Mfuko ulikutana na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kujadiliana namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana na kuwafanya wastaafu wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na kuweza kutengeneza ajira kwa vijana. 
 
“Lengo likiwa SIDO iwajengee uwezo kitaalamu na kuwapatia vifaa ili wastaafu wa PSPF waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na shughuli nyingine za uzalishaji.” Alisema Bw. Mayingu. 
 
Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kzuingatia ukweli kuwa, katika kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua kuwa baadhi yao hujiingiza katika biashara mbalimbali ambazo hawakujiandaa vema na matokeo yake kupoteza mafao yao.
 Washiriki wakijadiliana
 Mkurugenzi wa Masoko wa wa Mfuko wa uwekezaji wa pamoja UTT-AMIS, Daudi Mbaga, akitoa mada ya namna wanachama wa taasisi hiyo wanavyoweza kufaidika kwa kuwekeza kwenye Mfuko huo.
 Mshiriki akizungumza kwenye semina hiyo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili
 Mmoja wa wastaafu wa PSPF, ambaye kwa sasa ni mteja wa benki ya NMB, akitoa ushuhuda jinsi alivyofaidika baada ya kuitumia benki hiyo pale alipostaafu ambapo sasa anaedesha miradi mbalimbali kufuatia mikopo anayompewa na benki hiyo na kumfanya aishi maisha ya amani.
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), Mkurugezni wa Uendeshaji, Bi.Neema Muro, (katikati) na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Silayo, wakifurahia michango ya mawazo kutoka kwa washiriki wa semina.
 Meneja wa Mfunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo SIDO, Bi. Beata Minga, (kulia), akiongoza kikao wakati wa kufungwa kwa semina ya siku mbili ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
 Mshiriki akichangia mawazo yake kwenye semina hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (katkati), akiwa na viongozi wengine wa Mfuko kutoka kushoto ni Meneja Mipango na Utafiti, Bw.Luseshelo Njeje, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Sulayo, na Meneja wa Pensehini za Wastaafu, Bw.Mohammed Salim.
Bw. Mayingu, (kushoto), akijadiliana jambo na Bwana Dominic Haule, Mkurugenzi IMADS, (wakwanza kulia), wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bi. Neema Muro, Bw. Gabriel Silayo, Bw.Bw.Luseshelo Njeje na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kufungwa kwa semina hiyo
 Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye awali aliifungua rasmis semina hiyo, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (watatu kulia waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw.John Mongella, (watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (wapili kulia), na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, viongozi wengine na wafanyakazi wa PSPF
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro wakiwasili ukumbini
 Naibu waziri wa fedha na mipango, Dkt. Asshatu Kijaji, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. Nyakimuro Muhoji (katikati) na Mkurugenzi Mkuu, Bw. dam Mayingu wakiwasili ukumbini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »