NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka wilaya
zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu hivi
karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha kujiandaa
kustaafu kwa amani.
Katika
semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha BoT
Capri-point jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha nao
wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao
wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
Wadau
hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na
Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO.
Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCBBi Doris Mlenge, Afisa Masoko wa Mfuko wa UTT-AMIS, akiwapatia vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo. “Kwa mtu yeyote anayetegemea kupata kipato kwa mkupuo kutokana na pensheni au chanzo kingine cha fedha anatakiwa kuwekeza kwenye Mfuko huo ili aweze kupata kipato cha mara kwa mara na akasema kuwekeza kwenye mifuko ya kujikimu kama UTT-AMIS kunatoa faida kubwa ukilinganisha na uwekezaji wa namna hiyo kwenye masoko ya fedha.
Bw. Denis Mwoleka, ambaye ni Meneja wa CRDB tawi la Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza, akizungumza kuhusu umuhimu wa wastaafu hao watarajiwa kujiunga nabenki hiyo kwa kutarajia kupata faida mbalimbali ikiwemo huduma mpya ya akaunti ya akiba ya dhahabu ambayo ni njia rahisi ya kujiwekea akiba ili kufanikisha malengo ya baadaye.
Afisa kutoka Shirika la viwanda vidogo vidogo SIDO, akihamasisha wastaafu watarajiwa kuwekeza kwenye uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawawezesha kujikimu kimaisha na ksutaafu kwa amani. yeye alsiema SIDO iki tayari kutoa ushauri na mafunzo ya uanzishaji wa viwanda hivyo
Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim,(kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wapili kushoto) na Meneja Mipango na Utafiti wa Mfuko huo, Bw.Luseshele Njeje
Meneja wa Fedha wa PSPF, Bw.Lihami Masoli. (kulia), na Mtafiti Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw.Mapesi Maagi, (katikati), wakibadilishana mawazo na Katibu Msaidizi wa TSC wilaya ya Kwimba, Bw. Fundikira R.K. James, wakati wa mapumziko ya semina hiyo
Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim, (kushoto), akifafanua mambo kadhaa kuhusu pensheni
Bw. Silayo (kushoto), akiteta jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi
EmoticonEmoticon