Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa
habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi
zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi,
Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi
Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe
Kigoma (CCM), Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na
Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi
wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada
inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi
iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za
Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi
wa Mpango huo.
Sehemu ya Wawakilishi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini pamoja na
Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa
Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania).
Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia
Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi
zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha
ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi,
Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na
Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati
wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi
Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon