Mfuko
wa Taifa wa Bima ya afya NHIF umezindua mpango wa madaktari Bingwa
Mkoani Geita lengo likiwa ni kushirikiana na serikali kupunguza
changamoto za upatikanaji wa huduma za kibingwa na kusogeza huduma
karibu na wananchi pamoja na wanachama wa mfuko huo.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi
NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba amesema watu elfu kumi na tatu mia
moja na sitini na saba (13167) na kati ya hao mia nne sitini(460)
wamekwisha kufanyiwa huduma ya upasuaji.
“Kabla
ya kuleta madaktari bingwa kwenye Mkoa husika mfuko huwa unafanya
tathimini na kubaini uhitaji katika kila Mkoa ndivyo hivyo tumefanya
kwenye Mkoa huu wa Geita na kuamua kuleta madaktari bingwa kama ambavyo
nimeeleza kwa hiyo Tumekuja na madaktari Bingwa pamoja na Dawa na
mashuka ambavyo vitasaidia kwenye huduma za kiafya”Alisema Mramba.
Aidha
Bi, Mramba ameongezea kuwa matarajio ya mfuko huo ni kupunguza
msongamano wa wagonjwa katika hospitali za ngazi ya juu ikiwa ni pamoja
na kutoa fursa kwa madaktari kutoa huduma kwa uhakika zaidi kwa watu
wachache watakaolazimika kufuata huduma hizo kwenye hospitali Kubwa
ikiwa ni pamoja na watumishi wa Hospitali husika kutumia fursa ya
kujifunza kwa kupata ujunzi na utaalamu kupitia kwa madaktari wageni.
Kwa
Upande Wake Mgeni Rasmi Ambaye ni Katibu Tawala Mkoani Humo Celestine
Gesimba amewata madaktari kuwatumia madaktari bingwa waliofika
Hospitalini hapo kutoa huduma kwa wagonjwa ili kujifunza mbinu mpya za
utoaji wa huduma badala ya kwenda kufuata mbinu hizo nje ya maeneo yao
ya kazi
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando Dr
Neema Chami amesema tangu kuanza kwa huduma hizo kwa siku 2 sasa
wamewahudumia watoto 80 hali inayoonesha mafanikio ya lengo la wao
kufika mkoani humo.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita Dr Brian Mawala amesema ombi la
Wananchi la kutaka Madaktari Bingwa wawe wanafika mara kwa mara
Hospitalini hapo, litafanyiwa kazi kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya, NHIF ili kupunguza wananchi wasisafiri umbali mrefu kufuata huduma
za Kibingwa
Zoezi
la utoaji wa huduma za upasuaji kutoka kwa Madaktari Bingwa kwenye
Mikoa ya Geita na Kigoma lilianza rasmi Mei 22 siku ya jumatatu kwa
uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ambapo hadi sasa ni
jumla ya wagonjwa 1,204 wamekwisha hudumiwa kwa siku mbili huku
wagonjwa ambao wamefanyiwa upasuaji kwa mikoa miwili ni kumi na nne.
EmoticonEmoticon