Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa akizungumza wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu katika Jiji la Arusha
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bi. Eunice Tondi akisoma taarifa katika
maadimisho ya juma la Elimu yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Arusha
School jijini hapa.
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu
Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa(kwanza kushoto)
akitembelea maonyesho wakati wa Juma la Elimu lililofanyika katika
viwanja wa Arusha School.
Wanafunzi wa shule mbalimbali pamoja na walimu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa sherehe za Juma la Elimu
Katibu
Tawala wa Wilaya David Mwakiposa(kushoto) akikabidhi Kombe la Ushindi
kwa kuwa nafasi ya kwanza kimkoa kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya Lucky Vicent
Bw. Innocent Mushi.
Katibu
Tawala wa Wilaya David Mwakiposa(kushoto) akikabidhi cheti cha Ushindi
kwa kuwa nafasi ya kwanza kiwilaya kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya Lucky
Vicent Bw. Innocent Mushi.
Wanafunzi wa darasa la nne wakifurahi maadhimisho ya Juma la Elimukatika viwanja vya Arusha School.
…………………………………………………………………………………..
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Shule ya msingi Lucky Vicent
yaibuka na mshindi wa Jumla Kitaaluma kwa kushika nafasi ya kwanza
Kimkoa katika maadimisho ya Juma la Elimu yaliyoadhimishwa katika
viwanja vya Arusha School jijini hapa.
Shule hiyo iliyopata na msiba wa
wanafunzi 32, walimu 2 pamoja na dereva kutokana na ajali ya Coastal
hivi karibuni imefanya vizur katika mitihani ya darasa la saba
iliyofanyika mwaka 2016 katika ngazi ya Mkoa na Wilaya hivyo
kujinyakulia Kombe pamoja na Cheti.
Akipoka zawadi hizo za Ushindi
Mwel Mkuu wa Shule hiyo Bw. Innocent Mushi alisema wanafarijika kupata
zawadi hizo ingawa bado simanzi na majonzi yametanda shuleni kwa
wanafunzi pamoja na uongozi wa shule hiyo.
“Tunamshkuru Mungu kwa Shule yetu
kufanya vizuri na hizi ni jitihada za walimu kufanya kazi kwa bidii
pamoja na wafunzi kuzingatia yale wanayofundishwa na walimu wao hakika
zawadi hizi zimetupata faraja katika kipindi hiki kigumu tunachopitia.”
Alisema Mwl. Mushi.
Katibu Tawala wa Jiji la Arusha
Ndg. David Mwakiposa ambaye ndiye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
amepongeza shule zote zilizofanya vizuri Kitaaluma kwa mwaka uliopita
ikiwa ni pamoja na Walimu na Wanafunzi na pia alitembelea miradi ya
kiubunifu inayoendeleza sanaa za wanafunzi ikiwa ni pamoja na
kuwawezesha kupata ajira hapo baadae.
Mwakiposa alisema “Taifa lolote
haliwezi kuendelea pasipo wananchi wake kuelimika hivyo nichukue fursa
hii kuweka msisitizo kwa walimu na viongozi mbalimbali katika sekta ya
elimu kufundisha wanafunzi kwa weledi na kutoa elimu bora ili malengo
mbalimbali ya kitaaluma yaweze kufikiwa”
Pia aliongeza kwa kusema kuwa
amefurahishwa na kuhamasishwa sana katika maonyesho yaliyofanywa na
wanafunzi hasa maonyesho ya mafunzo ya kitaaluma, kisayansi na ufundi
stadi na kusisitiza kuwa endapo watashirikisha jamii taaluma
walizofundishwa na walimu wao na wakiwezeshwa na wadau wa elimu basi
Tanzania yetu itapiga hatua kubwa hasa katika suala zima la uchumi wa
viwanda.
Miongoni mwa maonyesho yaliyoweza
kuonyeshwa na wanafunzi wa kawaida na wenye ulemavu ikiwemo viziwi,
matatizo ya akili na wasioona ni pamoja na utaalamu wa kusindika
maparachichi na kutengeneza mafuta yanayoweza kutumika kama kilainishi
katika karakana za vyuma vyenye kutu na dawa ya ngozi, ujuzi wa
kutengeneza dawa ya kung’arishia viatu pamoja na ushonaji wa nguo na
vitambaa vya kupambia majumbani.
Pia wanafunzi walionyesha namna
ya kuzalisha umeme kwa kutumia nyaya, utengenezaji wa mapambo kwa
kutumia shanga zinazotokana na makaratasi na watoto wenye ulemavu wa
kusikia wanavyoweza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA)katika kujifunza mambo mbali mbali.
Maadhimisho ya Juma la Elimu
hufanyika kila mwaka lengo ikiwa ni kutathimini ubora wa Elimu,
kuwatambua waliofanya vizuri kitaaluma na kuonyesha kwa vitendo ubunifu
wa wanafunzi na sanaa inavyokua katika sekta ya Elimu.
EmoticonEmoticon