- Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron (wa pili kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akishuhudia.
- Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akiwa katika mkutano huo.
- Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron akifafanua jambo katika uzinduzi wa 'NMB FANIKIWA ACCOUNT'. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard (kushoto).
BENKI ya
NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati
ijulikanayo kama 'NMB FANIKIWA ACCOUNT' ili waweze kukua kibiashara
pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa
akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti
magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka
wafanyabiashara wote kuitumia.
Alisema
kuwa NMB imebuni akaunti hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya
wafanyabiashara wadogo kukosa mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye
mikopo. Akifafanua zaidi juu ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara,
James Meitaron alisema Benki ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika
kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha
katika kuendeleza biashara zao.
Alisema
Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na
taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara
wadogo na wakati wakiwemo 'mama lishe'.
- Mkutano huo ukiendelea.
- Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki ya NMB kushoto.
EmoticonEmoticon