Serengeti
Boys - Timu ya Taifa ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka
17, kesho Jumapili Mei 21, mwaka 2017 inarusha karata muhimu katika
mchezo hitajika dhidi ya Niger kuwania nafasi ya kucheza fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika - AFCON u-17.
Serengeti
Boys itaingia Uwanja wa Port Gentil hapa mjini Port Gentil huku mkononi
ikiwa na pointi 4 ilizovuna katika michezo yake miwili ya awali kwani
ilianza kupata sare tasa dhidi ya Mali Mei 15, mwaka huu kabla ya
kuifunga Angola Mabao 2-1 katika mechi zilizofanyika Uwanja wa l’Amitee
jijini Libreville.
Vijana
wa Serengeti Boys ambao wamefikia Hoteli ya Strange Complex, wana ari
ya ushindi dhidi ya vijana wenzao wa Niger ambao wana alama moja
waliyoipata kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya Angola walipocheza
mwanzoni mwa wiki hii. Niger walipoteza mchezo wa pili dhidi ya Mali.
Walifungwa mabao 2-1.
Kocha
Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime amesema: “Huu ni mchezo
muhimu wa kupata matokeo muhimu kwa vijana wetu. Tumejiandaa vema
kuwania nafasi ya angalau kuingia nusu fainali.”
Shime
ambaye wakati wote amekuwa akishukuru uongozi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), kwa namna unavyojitoa kuiandaa timu hiyo kwa
kuipa kambi tulivu nchi mbalimbali, amesema: “Hili ni deni.”
Akifafanua
zaidi, Shime ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi,
anasema: “…Nina deni. Nadaiwa na uongozi wa TFF chini ya Jemedari Jamal
Malinzi, pia nina deni kwa Watanzania ambao wamekuwa wakihaha kutuombea
dua na kuichangia timu hii.
“Nawashukuru
sana kwa namna wanavyojitolea kwetu, na ndio maana nasema hili ni deni
na niwaahidi tu kwamba nitaendelea kulilipa kesho kwa matokeo mzuri.
Katika kila mchezo huwa na mipango yangu na mpango wa kesho ni ushindi
tu. Tutacheza soka la kushambulia.”
Shime
ambaye alisema kwamba ataingia kwa mfumo mwingine kesho, hatarajii
kikosi chake kikawa na mabadiliko makubwa labda mpaka atakapoangalia
mazoezi yatakayofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja Sogara.
Nahodha
wa timu hiyo, Dickson Job aliwatoa shaka Watanzania akisema vijana wote
wako vema kwa ajili ya mchezo huo kwani mpira wa miguu kwao ni ajira
kwa manufaa ya yao binafsi, familia kadhalika taifa ambalo limewatua
Gabon kutafuta Kombe la Mataifa ya Afrika.
“Kuna
watu wanadhani tunapochukuliwa na watu wa doping ni kama tunatumia
dawa, hapana. ni utaratibu wa mechi za kimataifa kwamba mara baada ya
mchezo wowote wa kimataifa, kanuni zinaruhusu madaktari kuchukua
wachezaji kadhaa na kuwapima ili kuandika ripoti ya kila mchezo.
“Mchezo
wa kwanza dhidi ya Mali nilichukuliwa mimi na Israel Patrick Mwenda na
wachezaji wa Mali wawili. Mchezo wa pili alichukuliwa Abdul Suleiman na
Kelvin Naftal na wenzetu wa Angola wawili. Ni jambo la kawaida ni ni
utaratibu kwa kitengo cha Doping,” alifafanua Job.
Serengeti
Boys inahitaji sare ya aina yoyote ili iwezi kuvuka ilihali Niger
ambayo ina alama moja na ikishika mkini, imejiwekea matumaini ya kusonga
mbele ikitamba kwmaba itafunga Tanzania.
Hakuna
shaka kuwa dua za Watanzania zitakuwa pamoja na timu nzima ya Serengeti
Boys ambayo kwa sasa imekuwa ikichungwa na timu pinzani katika kuwania
nafasi hii muhimu ya ujio mpya wa mpira wa miguu wa Tanzania.
Mungu Ibariki Serengeti Boys.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Barki viongozi wote wa Tanzania.
Mungu Bariki michuano ya CAF.
EmoticonEmoticon