OMPR, Jordan
Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania imejenga uwezo zaidi wa kukabiliana na vitendo
vya rushwa katika azma yake ya kujenga uchumi imara utakaostawisha Taifa
kwa kuongeza Mapato kupitia Sekta ya Utalii sambamba na Ujenzi wa
Viwanda vipya vya kudumu.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi anayemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John
Pombe Magufuli kwenye Jukwaa la Dunia la Uchumi { world Economy Forum }
wakati akiwasilisha Muelekeo wa Tanzania katika uimarishaji wa Sekta ya
Utalii hapo katika Ukumbi wa Mfamle Hassan Bin Talal pembezoni mwa
Bahari Nyeusi Mjini Amma Nchini Jordan.
Balozi
Seif alisema zipo jitihada za ziada zilizochukuliwa katika ujenzi wa
miundombinu ndani ya Sekta ya Utalii kutokana na Rasilmali nyingi
zilizopo ikiwemo Mbuga za Wanyama, Ardhi yenye Rutba, Fukwe za kuvutia
pamoja na Mlima wa Pili kwa urefu Duniani Kilimanjaro zilizoifanya
Tanzania kujikita zaidi katika uimarishaji wa Seklta hiyo.
Alisema
Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya
Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikichukuwa juhudi mbali mbali kwa
kushirikiana na Sekta na Taasisi Binafsi kuendeleza Viwanda na soko la
Biashara ya Utalii lenye muelekeo mkubwa wa kutoa ajira hasa kwa Vijana
wanaomaliza masomo yao ya Sekondari na Vyuo Vikuu.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza washiriki wa Warsha hiyo ya
mambo ya Utalii ndani ya Jukwaa la Dunia la Uchumi Mjini Amman Jordan
kwamba Tanzania tayari imeimarika katika kukabiliana na matukio ya
Kigaidi ili kutoa nafasi kwa Wawekezaji wa Kimataifa kutumia fursa
zilizopo Tanzania katika kuwekeza miradi yao hasa ile ya Utalii.
Alieleza
kwamba Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hivi sasa inaendelea kuwa
kisiwa cha Amani ndani ya Mwambao wa Afrika Mashariki na Ukanda wa
Kusini ya Afrika ya Jangwa la Sahara kutokana na ushiriki wake uliojaa
nidhamu katika ulinzi wa maeneo hayo.
Alisema
kutoka na hali hiyo ya amani na utulivu iliyopo Nchini Tanzania
Makusanyo ya mapato kupitia sekta ya Utalii yanakadiriwa kufikia
Shilingi Bilioni 1.6 licha ya kukumbwa na changamoto ya mabadiliko ya
tabia Nchi pamoja na kutumia Teknolojia ya Habari katika kuutangaza
Utalii nje ya Nchi. Akifafanua Sekta ya Utalii kwa upande wa Visiwa vya
Zanzibar Balozi Seif alisema Sekta hiyo ambayo kwa sasa imechukuwa
nafasi ya Tatu katika Uchumi wa Dunia imekuwa tegemeo kubwa la Uchumi wa
Zanzibar.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba tokea kuimarishwa kwa fursa za Uwekezaji
katika Sekta ya Utalii Zanzibar mwanzoni mwa Miaka ya 80 zipo fursa
nyingi za ajira zinazokadiriwa kufikia Laki 376,000 rasmi na zile zisizo
rasmi na kuleta faraja kwa Wananchi walio wengi.
Alisema
Lengo la Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo ni kufikia fursa za ajira zipatazo Laki
500,000 hadi ifikapo mwaka 2020. Balozi Seif alieleza bila ya shaka
kwamba Utalii kwa sasa imekuwa Sekta muhimu katika ukuaji wa Uchumi
Kidunia uliopanda na kufikia kiwango cha asilimia 9% kinachokisiwa
kugharimu Dola za Kimarekani Trilioni 1.3 katika bidhaa zinazosafirishwa
kutokana na Sekta hiyo.
Alisema
rikodi ya Bara la Afrika ya Watalii Milioni 14.8 ndani ya Mwaka 2000
imeongezeka hadi kufikia Milioni 68 kwa Mwaka 2015 ikifikia asilimia 62%
ya idadi ya wageni wa nje wanaoingia Bara hilo walioibua ajira zipatazo
25,000,000 sawa na asilimia 7.1% ya ajira zilizoibuka ndani ya Bara
hilo. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania aliipongeza Jordan chini ya Kiongozi wake Mfalme
Abulla wa Pili kwa uamuzi wake wa kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa
Jukwaa la Dunia la Uchumi .
Jordan
imekuwa mwenyeji wa Jukwaa la Dunia la Uchumi { World Economy Forum }
kwa takriban mara Tisa sasa na 16 kwa Kanda na Mashariki ya Kati ya
Kaskazini mwa Afrika Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum -
WCF} limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake
Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland likilenga kusaidia kuepuka
vita sambamba na kupunguza wimbi la Wakimbizi katika eneo la Mashariki
na Kati na Kaskazini ya Bara la Afrika.
EmoticonEmoticon