Na Afisa Habari Mufindi
Halmashauri
ya Wilaya ya Maufindi imeendelea kutekeleza sera ya serikali ya
kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati kwa kuzindua na kuweka mawe
ya msingi kwenye zahanati za Vijiji vinne kati ya vitano zilizopo kata
ya Ihalimba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Uzinduzi
na uwekaji wa mawe ya msingi umetekelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo Mh. Festo Mgina, Diwani wa kata Ihalimba Mh. Award Mahanga sanjari
na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Prof. Riziki Shemdoe.
Taarifa
hiyo imevitaja vijiji vilivyo nufaika na huduma hiyo muhimu kwa usatawi
wa afya ya jamii kuwa, ni pamoja na Kijiji cha Wamimbalwe uwekaji wa
Jiwe la msingi, uzinduzi wa Zahanti ya Kijiji cha Vikula, uzinduzi wa
zahanati ya Kijiji cha Nundwe pamoja na uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye
azahanati tarajiwa ya Kijiji cha Ihalimba.
Awali
akiwahutubia wakazi wa Vijiji hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Festo
Mgina, alitoa rai kwa wananchi kujiepusha na tabia hatarishi
zinazochochea maambukizi ya Virusi vya ukimwi huku akiutaja Mkoa wa
Iringa kuwa na asilimia kubwa ya maabukizi ya 09.1 wakati asilimia ya
kitaifa ni 05.6 Pekee.
Aidha,
Kiongozi huyo mwenye dhamana ya juu ya uongozi katika halmashauri hiyo,
amekemea vitendo vya ubakaji kwa Watoto ambavyo vinashamili kwa kasi
Wilayani Mufindi.
Mnamo
mwaka 2015 wakati wa ufunguzi wa Bunge la Tanzania, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanazania Mh. Dk. John Pombe Magufuli, aliahidi kuwa
serikali ya awamu ya Tano itahakikisha sera ya kuwa na zahanati kwenye
kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata inatekelezwa kwa vitendo.

EmoticonEmoticon