WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA TAARIFA YA HALI YA VYOMBO VYA HABARI NCHINI TANZANIA KWA MWAKA 2016

May 03, 2017
Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, ambaye amemwakilisha Rais John Pombe Magufuli.
#BMGHabari
Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia), akizindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016". Kushoto ni mjumbe bodi ya Misa Tanzania, Lilian Lucas.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Uzinduzi wa "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016".
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua "taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016" kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.
Akizungumza mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na kulinda uhuru wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za uchunguzi huku akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi badala ya habari za kihisia.
Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba taarifa hiyo imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari Mosi hadi Disemba 31, 2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama wa SADC.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »