Alphonce Simbu Balozi wa DStv na
Mshiriki pekee kutoka Tanzania aliyeshiriki mashindano ya London
Marathon yaliyofanyika leo jijini London ameibuka mshindi wa tano huku
akivunja rikodi yake kwa kutumia muda wa 2:09.10 ambao ndio muda wake
bora zaidi tangu aanze kushiriki mashindano ya kimataifa. Kabla ya hapo
rekodi yake ilikuwa muda wa 2:09.21aliyoiweka mwaka jana kwenye
mashindano ya Lake Biwa Marathon nchini Japan.
Simbu ambaye ni mshindi wa medali
ya dhahabu wa Mumbai Marathon ameonyesha umahiri mkubwa katika
mashindano hayo hasa ikizingatiwa kuwa mashindano hayo yalikuwa
yanashirikisha vinara wengi wa riadha ulimwenguni wakiwemo Muethiopia
Kenenisa Bekele wakenya Daniel Wanjiru, Bedan Karoki na Abel Kirui.
Mara baada ya ushindi huo salamu
za pongezi zimekuwa zikimiminika huku mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice
Tanzania Maharage Chande akisema kuwa kampuni yake imeridhishwa sana na
ufanisi aliouonyesha katika mashindano hayo. Amesema uwekezaji
uliofanywa na kampuni hiyo katika kumdhamini Simbu umezaa matunda kwani
kiwango cha mwanariadha huyo kimekuwa kikiimarika siku hadi siku.
“Tumefurahishwa sana na kiwango alichoonyesha Simbu kwenye London
Marathon. Hii ni ishara nzuri sana na tunaamini atafanya vizuri zaidi
kwenye mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London mnamo
mwezi Agosti mwaka huu”
Kwa upande wake, meneja wa
mwanariadha huyo Francis John amesema kuwa ameridhishwa na kiwango
alichoonyesha Alphonce Simbu na kwamba punde tu atakaporejea wataanza
maandalizi kwa ajili ya ushiriki wake katika mashindano ya Dunia
yatakayofanyika mwezi agost mwaka huu.
Katika mashindano hayo nafasi ya
kwanza imechukuliwa na Mkenya Danie Wanjiru (2:05:48) akifuatiwa kwa
karibu na Kenenisa Bekele (2:05:57) na Bedan Karoki (2:05:41)
EmoticonEmoticon