Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe kuzindua Televisheni
ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.Televisheni
iyo itaonyesha kazi mbalimbali za Wizara,Taasisi na Idara za
Serikali.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Anastazia
Wambura.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake Anastazia
Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara
ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas wakifurahi mara baada ya kuzindua
Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe akizungumza na menejimenti ya Wizara
ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo(Hawapo Pichani) na kuipongeza
Idara ya habari kwa kuwa wabunifu.Kulia kwake ni Naibu Waziri wake
Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi
Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akiangalia mahojiano yaliyofanyika
kati ya Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo Hassan Abbas na Makamu wa Rais
Mhe.Samia Hassan Suluhu kuhusu maadhimisho ya Muungano yatakayofanyika
mjini Dodoma.Mahojiano hayo ni ya kwanza kupitia televisheni ya
mtandaoni ya Idara ya habari-MAELEZO.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.
……………………………………………………………………..
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza Idara ya Habari-MAELEZO
kwa ubunifu mkubwa katika kuitangaza Serikali.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo
jana mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya mtandaoni ya Idara ya
Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.
“Napenda nichukue fursa hii kwa
kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara
hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya
mtandaoni ya Idara hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Wizara
yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na” Alisema Waziri Mwakyembe.
Amesema kuwa kwa kazi ya kwanza
ambayo imeonekana katika televisheni hiyo imeonyesha weledi wa hali ya
juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara hiyo kuiga mfano mzuri na
kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina vipaji na ubunifu wa hali
ya juu ikiwemo timu yetu ya Vijana ya Serengeti Boys na n.k
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Habari-MAELEZO,amesema kuanzishwa kwa televisheni hii ya
mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko
mbalimbali na uzinduzi wake wa mapema utasaidia kufikisha taarifa
mbalimbali kwa jamii husika.
“Sisi kama Serikali tumekuwa
makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na hii
televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima
ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake”,Aliongeza Dkt
Abbas.
Mbali na hayo amesema kuwa
kipindi cha kwanza kabisa kuwekwa katika televisheni hii itakuwa
mahojiano ya maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya muungano waliyofanya
na Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Hassan Suluhu.
EmoticonEmoticon