Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa
Wanachama Bw. Ramadhani Mkeyenge akizungumza na Waandishi wa Habari
kuhusu dhana nzima ya utaratibu wa uwekaji akiba kwa hiari kwenye Mfuko
wa Pensheni wa LAPF kwenye mkutano uliofanyika Makao makuu ya Mfuko
mjini Dodoma .
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na
waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya
teknolojia ikiwemo huduma za M-pesa na Tigo-pesa katika kuwafikia
Watanzania walio wengi ili wajiunge na kuweka akiba kupitia “LAPF Jiongeze Scheme”.
Meneja mwenye dhamana na Skimu ya uchangiaji wa hiari (LAPF Jiongeze Scheme)
Bi. Hanim Babiker akizungumzia taratibu mbalimbali zinazotakiwa
kufuatwa ili kuweka akiba kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa wakati wa
Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma.
Afisa huduma kwa wanachama wanaoweka akiba kwa hiari (LAPF Jiongeze Scheme)
Bw. Juma Venerando akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi Mfuko
wa Pensheni wa LAPF ulivyojipanga kuendelea kuboresha zaidi huduma kwa
wanachama.
Mwakilishi wa Kampuni ya Tigo
Mkoani Dodoma Bw. Gideon Morris akizungumza na waandishi wa Habari
jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha ubora
zaidi wa huduma zao za Tigo-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote
kuweka akiba ya hiari Kwenye Mfuko wa LAPF.
Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom
Mkoani Dodoma Bw. Balikulije Mchome akizungumza na waandishi wa Habari
jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha ubora
zaidi wa huduma zao za M-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote
kuweka akiba ya hiari katika Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo
mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo mbalimbali yaliyotolewa
kwenye utambulisho wa huduma za uwekaji wa akiba ya hiari kwa njia ya
M-pesa na Tigo-pesa kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF, mkutano
uliofanyika mjini Dodoma.
EmoticonEmoticon