WAFANYABIASHARA WA VILEO KATIKA MANISPAA YA UBUNGO WATAKIWA KUWASILISHA MAOMBI YA LESENI KABLA YA MACHI 15, 2017

March 10, 2017

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo anawatangazia wafanyabiashara wote wa vileo kuwa msimu wa kukata leseni za biashara za vileo kwa mujibu wa sheria ya vileo Na 28 ya Mwaka 1964 na marekebisho yake unaanza tarehe 1/04/2017.

Hivyo kila mfanyabiashara anapaswa kuwasilisha maombi ya leseni za vileo katika ofisi ya Biashara Manispaa ya Ubungo zilizopo eneo la Kibamba CCM Kabla ya tarehe 15/03/2017. (Maombi yaambatanishwe na Tax Clearence Certificate na Leseni iliyoisha)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »