SBL mdau muhimu wa maendeleo kiuchumi, asema Mkuu wa Mkoa Mwanza

March 09, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(katikati) akionyesha kwa waandishi wa habari bia mpya ya chapa Allsopps   ambayo  inauzwa katika soko la Afrika mashariki., kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na Meneja kiwanda Dominic Mkemangwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akifafanua jambo jijini Mwanza jana wakati wa uzinduzi wa bia mpya ya Allsopps, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.

Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi wa bia chapa Allsopps  ambayo  inauzwa katika soko la Afrika mashariki.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL  na waandishi wa habari mara baada wa bia chapa Allsopps  ambayo  inauzwa katika soko la Afrika mashariki.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiongozana naviongozi wa SBL na  waandishi wa habari  maeneo ya kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza mara baada ya uzinduzi wa wa bia chapa Allsopps  ambayo  inauzwa katika soko la Afrika mashariki.

Mwanza, Machi 8, 2017- Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  leo ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuzalisha bidhaa zenya ubora wa hali juu jambo ambo limiweizesha kampuni hiyo kushinda tuzo mbalimbali za ubora ndani na nje ya nchi.
 Mongella alitoa  kauli hiyo  wakati alipokitembelea kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza  ambako pia  aliipongeza kampuni  kwa mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi kupitia uzalishaji   wa ajira, ulipaji  kodi na hali kadhalika programu za kusaidia jamii.
 “SBL ni mdau  katika ajenda ya maendeleo ya nchi yetu. Kama serikali tutajaribu  kuanzisha mazingira  ambayo yanawezesha  biashara  kama hii ili  istawi vizuri na kuvutia uwekezaji pia,” alisema Mongella.
 SBL inazalisha  chapa za bia  ambazo ni Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick na hali kadhalika kusambaza  pombe kali zinazofahamika  duniani  ambazo zinazalishwa na  kampuni yake  uwekezaji  Diageo.
 Mwezi uliopita  Kiwanda cha SBL cha Mwanza kilianza uzalishaji wa bia chapa Allsopps  ambayo  inauzwa katika soko la Afrika mashariki.
“Hatua ya kuzalisha Allsopps katika kiwanda chetu cha Mwanza  ni sehemu ya mbinu ya uendeshaji kikanda  ya EABL. Hili limekuwa na matokeo ya kunufaisha  kwa masoko yote  na kwa biashara yetu,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha.
Kwa mujibu wa Wanyancha, SBL inaendesha  miradi kadhaa ya kuisaidia jamii  nchi nzima katika  maeneo ya upatikanaji wa maji, utoaji wa  elimu- ambapo wanafunzi walio na  weledi mkubwa kutoka mazingira yenye uhitaji  hupatiwa udhamini wa masomo kwa ajili ya kusomea  kozi za shahada ya kwanza katika vyuo vikuu vya ndani  na hali kadhalika kampeni ya  Ukiwa Umekunywa Usiendesha gari  ambayo inahamasisha unywaji wa kistaarabu

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »