Tigo yatangaza washindi wawili wa shindano la Digital Changemakers, yawazawadia dola 40,000 jijini Dar Es Salaam leo

March 10, 2017
 Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni Meneja Programu  wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka na Meneja Huduma za jamii(CSR) Tigo , Halima Okash.


 Meneja wa Programu wa Reach For Change, Josephine Msambichaka akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi  kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers.

Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akiongea na wageni waalikwa kwenye hafla ya makabidhiano.


Mshindi wa  shindano la Tigo Digital Changemakers,Sophia Mbega akiongea na wanahabari mara baada kukabidhiwa hundi ya dola za kimarekani elfu 20 jijini Dar Es Salaam leo, Pichani nyuma ni Mshindi wa shindano hilo pia aliyejinyakulia pesa hizo, Nancy Sumari. Jumla ya washindi wawili walipata dola elfu 20 kila mmoja.

.Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Nancy Sumari (katikati)wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni kulia Meneja wa Programu wa Reach For Change, Josephine Msambichaka na Halima Okash.


Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Sophia Mbega (katikati)wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni kulia Meneja Programu  wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka, Halima Okash na mwisho kulia ni Nancy Sumari.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Diego Gutierrez akiongoea na wanahabari. wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa kila mmoja kwa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers leo, Tigo kushirikiana na taasisi ya Reach for change ndio waliondaa shindano hilo.Pembeni Meneja Programu  wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka na Meneja Huduma za jamii(CSR) Tigo , Halima Okash.




 Dar es Salaam, Machi 09, 2017-  Tigo Tanzania kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Reach for Change  imetoa tuzo ya dola za Marekani 20,000 kwa kila mmoja kwa washindi wawili  wa shindano la tano  la Kidijitali la Tigo la waleta mabadiliko (Tigo Digital Changemakers). Shindano hilo  linalenga  kuibua na kuwasaidia wajasiriamali jamii  ambao wanatumia programu na teknolojia katika kuboresha  jamii na kuleta mabadiliko kwa vizazi vijavyo. Pamoja na nyongeza katika msaada huo wa kifedha, washindi  wanapewa nafasi ya kutumia  kituo cha  Reach for Change  ambacho kinawapatia ushauri, utaalamu na  kuingia katika mitandao duniani ambayo itawawezesha kujenga ujasirimali  jamii  ulio endelevu kifedha utakaounda mabadiliko katika uwanja mpana.
Washindi wa mwaka huu katika tuzo hiyo ni Sophia Mbega  na Nancy Sumari. Sophia Mbega aliwavutia majaji  na mkakati wake mkubwa wa kidijitali  ambao umejielekeza katika  kuvisaidia  vikundi binafsi vya wanawake  maarufu kama VICOBA. Ameibuka na programu ya simu  ambayo inaunda  jukwaa la ushirikiano  linalotumia programu zilizopo kwa usimamizi wa kifedha na majukumu  katika njia ambayo  inaendana na mazingira ya Kiafrika. Kupitia programu hiyo, watumiaji wote, bila kujali sehemu wanayokuwepo  wanaweza kuhamisha fedha  kwenda katika akaunti  ya kikundi cha Vicoba (ikiwa ni moja kwa moja  kwa kutumia namba iliyo katika mfumo wa USSD), kuangalia rekodi zao zote za kifedha, faida iliyozalishwa, taarifa za wiki n.k.
Mkakati  ulioshinda tuzo wa Nancy Sumari  unajulikana KIDS JENGA HUB ambao unaangalia msingi wa uelewa wa watoto.  Kupitia mkakati huo wa  nafasi ya kuanza kuwashirikisha  watoto, anafundisha  program za kompyuta,  matumizi ya kiroboti  na stadi za kuweka namba  kwa wanafunzi wa  shule ya msingi.  Mkakati huo pia unawafunulia watoto katika kujifunza msingi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kama vile  stadi za kiprogramu ambazo matokeo yake  zinatumika katika malengo mengi ya kielimu na burudani.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  alisema, “ Ni kutokana na furaha hii kubwa  kwamba tunatangaza washindi  wa mwaka huu wa Shindano la Tigo la kidijitali la Waleta mabadiliko. Kwa mwaka wa tano sasa Waleta mabadiliko  wameyagusa  maisha ya watoto zaidi  250,000 nchini Tanzania  na tunaamini kwamba kwa nyongeza hii ya Waleta mabadiliko wawili  tutaleta mabadiliko  katika maisha ya watoto wengi zaidi na kusaidia kuifanya Tanzania  kuwa sehemu nzuri kwa  vizazi vyetu vijavyo.”
Gutierrez aliendelea kufafanua kwamba  kama nembo ya maisha ya kidijitali Tigo inatoa msukumo kwa mawazo na miradi inayoendeshwa  na teknolojia  ambayo yanaleta mabadiliko endelevu. “Teknolojia ya kidijitali sio tu inabadilisha namna ambavyo tunafanya  biashara ndani ya Afrika  bali pia  inaleta mapinduzi  kwa njia tofauti  na  kutatua masuala ya maendeleo ya jamii. Hivyo kutokana na heshima hii kubwa  ni kwamba kwa mara nyingine  tunaunda fursa  kwa  kwa mawazo hayo kutambuliwa, kuungwa mkono na kubadilisha hadi kiwango cha juu cha matokeo ya kijamii na kiuchumi,” alisema.
Huu ni mwaka wa tano  ambapo Tigo  na Reach for Change  wanatangaza washindi wa shindano hilo. Washindi walioingia fainali ambao huchaguliwa kutoka kundi la mamia ya  wajasirimali jamii  ambao wametumia programu za  kiteknolojia kupata suluhisho  kwa matatizo yanayoikabilia jamii ya Watanzania.
Gutierrez  aliwapongeza washindi waliotangulia  na papo hapo akitoa msukumo kwa  wengine  kushirikiana mawazo yao.
“Uchaguzi wetu wa wajasiriamali jamii  unavutia sana. Hadi sasa  tumeshasaidia  jumla ya waleta mabadiliko ya kidijitali jamii tisa (9) na tunatarajia kuwasaiidia  wajasiriamali jamii wengine  kila mwaka,  ili kufanya karakati hizi zisonge mbele.”
Waleta mabadiliko katika program hi ni pamoja na Faraja Nyalandu ambaye anaendesha  ujasiriamali jamii  kidijitali  unaofahamika Shule Direct. Shule Direct  inatoa mada za kielimu  kidijitali  kukabiliana na uhaba wa walimu na kuhakikisha  kila mtoto na  vijana wanapata elimu bora.  Asasi ya Faraja pia inatoa  programu ya simu  inayofahamika Makini SMS ambayo inawasaidia watoto kujifunza  kwa kutumia maswali ya kuchagua  masomo tisa. Hivi sasa  amepanga kuifanya  asasi hiyo kuwa ya kikanda.
Carolyne Ekyarisiima ni mleta mabadiliko ya kidijitali mwingine wa Tigo  ambaye anafanyika kazi  kuziba pengo la kijinsia katika  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia  ujasiriamali wake wa kijamii, Apps & Girls. Carolyne  ameleta mabadiliko kwa mamia ya watoto wa kike , kupitia  klabu za masomo shule, warsha, maonesho , kuweka kambi pamoja  na mashindano. Sio tu kwamba hii inasaidia  bali pia  inahakikisha  kwamba watoto wa kike  wengi  wanaweza kuzifikia  teknolojia za kidijitali. Hali kadhalika Carolyne amewawezesha kuwa  viongozi wa Tehama wa baadaye. Carolyne  hivi sasa anaupanua ujasirimali jamii wake  kuleta matokeo makubwa na kuwapatia wasichana walio wengi  elimu ya teknolojia  na kuwasaidia kuanzisha masuluhisho  kwa masuala ya kijamii  kupitia  kupitia programu zao za  kidijitali  na mitandao.
Joan Avit ni mleta mabadiliko mwingine  ambaye anaboresha  ubora wa elimu ya awali  kupitia ubinifu wa  kidijitali. Ubunifu wake unaofahamika GraphoGame  Tanzania unawapatia  kujifunza kupitia mchezo ambao ni rafiki kwa motto ambao  unawasaidia watoto  kujifunza kusoma  kwa kuzitambua  herufi. Ubinifu wake umebadilisha maisha kwa mamia ya wanafunzi wadogo ambao awali walikuwa na hali mbaya katika kujifunza lakini hivi sasa wanachanua kutokana na  ubunifu wake wa kidijitali.
“Tumekuwa tunaunga mkono kazi zote za waleta mabadiliko wetu  na mwaka huu  tumeangalia na  kuwaunga mkono wajasiriamali jamii wengine wawili   walio jasiri na wabunifu,” alisema Gutierrez.
Akizungumza hafla ya tuzo hiyo Meneja Programu  wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka alipongeza  ushirikiano wa asasi  hiyo na Tigo, akibainisha kwamba imetoa  fursa sahihi kwa utekelezaji wa  miundo ya biashara iliyoendelevu ambayo inanufaisha jamii  hususani  idadi kubwa ya watoto kote nchini.
Mwisho  


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »