Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake. (Picha zote na Nassir Bakari)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akielezea jinsi Bajeti ya Manispaa hiyo ilivyopitishwa kwa kuungwa mkono kwa 100% kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kilichofanyika 4/03/2017.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo imebainisha namna ya kuboresha maisha ya wakazi wake kwa kuweka
mpango mzuri wa muda wa kati wa mwaka 2017/2018 – 2019/2020 ambao unalenga kukuza uchumi, na kupunguza umaskini
ili kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa wananchi
wake.
Mpango huo umeandaliwa
kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, kwa mujibu wa sheria ya bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango
mkakati ni kutekelezwa kwa matokeo
makubwa sasa (BRN), Sera ya Taifa ya UKIMWI, Sera za kisekta, Mipango
Shirikishi Jamii ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ya Kata na Mitaa.
Hayo yamebainishwa na
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida na
ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018,
Makadirio yalijadiliwa na Waheshimiwa Madiwani katika Kamati za Kudumu,na
kuidhinishwa na baraza maalumu la madiwani jumamosi ya tarehe 04/03/2017 kwa katika Halmashauri ya Manispaa
ya Ubungo.
Mstahiki
Meya alisema kuwa ili kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango
huu umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa
ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi katika
maeneo yao.
Alisema kuwa
Mpango huo umejielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo
ya haraka (quick wins) ambayo yatasaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka katika
kipindi kifupi na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Ubungo.
Aidha
alieleza maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mpango huo kuwa ni pamoja na Kuboresha
na kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Manispaa, Ujenzi wa ofisi za makao makuu
ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Kuboresha miundombinu ya Afya, Shule za
Msingi na Sekondari, Kuboresha miundombinu ya maji, mifereji, taa za barabarani
barabara na Kilimo mjini, Kuboresha hifadhi ya mazingira na ukusanyaji wa taka,
Kuimarisha ushirikishwaji wa jamii katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya
maendeleo na Kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ndogo ndogo.
Katika harakati za
kuyafikia
mafanikio yaliyotajwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
ameeleza kuwa Manispaa hiyo Uimarisha mahusiano mazuri kati ya Serikali,
mashirika yasiyo ya Kiserikali na wadau wengine, Kuendelea kujenga uwezo na
ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma zilizo bora na haraka, Kuimarisha
Utawala bora, Uwajibikaji na Uwazi sambamba na Kujenga uwezo wa viongozi wakiwemo
Madiwani, Wenyeviti wa serikali za mitaa katika kusimamia shughuli za wananchi.
Sambamba na hayo
pia amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mwaka 2016/2017 ilikadiria kutumia Sh. 116,045,935,228.99 ikiwa ni
pamoja na fedha za mfuko wa barabara.
Kuanzia Julai hadi Disemba, 2016, Halmashauri ilikuwa imekusanya Sh.
1,024,839,737.74 fedha za vyanzo vya
ndani sawa na asilimia 8 ya maoteo ya Tsh
13,300,416,090.50 ya vyanzo vya
ndani yaliyotarajiwa kukusanywa kwa nusu mwaka wa bajeti yaani Julai 2016 hadi
Disemba 2016.
Katika
kipindi hiki Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeweza kutumia kiasi cha Sh. 150,764,997.88. ya makusanyo yake ya
ndani yaliyoanza kukusanywa mwezi Novemba
2016, na hakuna fedha yoyote ya
ruzuku iliyopokelewa hadi sasa kama inavyooneshwa katika Jedwali hapa chini.
Jacob ametaja changamoto mbalimbali zinazopelekea
ucheleweshaji katika kutoa huduma na kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwa ni
pamoja na Mwamko mdogo wa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo, Fedha za
miradi za Serikali kuu na wafadhili kutoletwa kwa wakati na hivyo kuathiri
utekelezaji wa miradi kama ilivyopangwa. Miradi yote iliyopangwa kutekelezwa
kwa fedha za ruzuku haijaanza, Makusanyo hafifu ya mapato ya ndani kutokana na
mgawanyo wa Halmashauri na upya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Hivyo
miradi iliyopangwa kutekelezwa kwa
mapato ya ndani mingi haijaanza kutekelezwa, Ukosefu wa maeneo ya kujenga
majengo mapya kama vile Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na Madai makubwa
ya fedha za fidia katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo Sababu zilizopelekea kukusanya mapato ya ndani chini ya malengo ni pamoja na Serikali
kuhamishia kodi ya Majengo kukusanywa na Mamlaka ya mapato TRA ambapo kwa wigo
wa makusanyo uliopo wa kodi ya majengo ni shilingi bilioni 6, kwa bajeti ya
mwaka 2016/2017 ya makusanyo ya ndani yenye makadirio ya Tsh. 26.6 bilioni, Kushuka
kwa mauzo ya wafanyabiashara hali inayopelekea biashara kufungwa na malipo ya
ushuru wa huduma kupungua, na SUMATRA kubadilisha route za mabasi ya kariakoo
(160) na mikoani (350) kimepunguza makusanyo katika kituo chetu cha Simu 2000
(Sinza bus terminal) ambapo takribani magari
kati ya 510 yaliyokuwa yanaingia kituoni yamepungua na kusababisha
upungufu wa Sh. 12,900,000/= kwa kila mwezi.
Sababu
zingine ni Upungufu wa vitendea kazi baada ya Mgawanyo wa Halmashauri na hasa
ukosefu wa magari yanayotumika kukusanyia mapato, Kipindi cha mpito tangu
kuanzishwa kwa Halmashauri hadi kuanza kukusanya mapato ya ndani kwa
Halmashauri yetu mpya ilipoanzishwa rasmi tarehe 1/07/ 2016, imeanza kukusanya
mapato yake ya ndani yenyewe kuanzia mwezi Novemba 2016, Walipakodi kuendelea
kulipia katika Halmashauri mama (Kinondoni) kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba
2016 kwa mazoea kiasi cha takriban Sh. milioni 500 kimekusanywa kimakosa na
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
mawasiliano yanafanyika ili kurejesha makusanyo hayo.
Ili kukabiliana
na changamoto hizo Mikakati ya Halmashauri imetajwa kuwa ni pamoja na Kuendelea
kutoa elimu na kuhamasisha wananchi ili kutambua kuwa miradi ya maendeleo
wanayochangia ni kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na vizazi vijavyo, Kendelea
kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya kwa mujibu wa
sheria na kuimairisha ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vilivyopo.
Mikakati mingine ni Kukusanya mapato yote kwa kutumia
mfumo wa kielektroniki, na Kununua maeneo ya pembezoni mwa mji na kuhakikisha
tunalipa fidia kabla ya kuyatwaa maeneo ya watu.
Vipaumbele vitakuwa katika maeneo yafuatayo:-Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob amebainisha kuwa Bajeti hiyo
imelenga katika kuboresha maisha ya wananchi na kukuza kipato cha mkazi ili
kukuza uchumi wa ndani ambapo ametaja vipaumbele 13 ambavyo vitapaswa kufanyiwa
kazi katika bajeti hiyo kuwa ni pamoja na Kuongeza ukusanyaji wa mapato ya
ndani kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, na Kuboresha utoaji wa huduma za afya
kwa kununua madawa na vifaa tiba na kuboresha miundo mbinu ya afya kwa kupanua
hospitali ya Sinza kwa kujenga ghorofa ya pili jengo la OPD, Ujenzi wa wodi ya
wazazi kituo cha afya mbezi, ujenzi wa jengo la kuhifadhia chanjo Mabibo, kujenga
zahanati ya King’azi Kwembe Jumla ya Tsh. 5,732,424,610.00 zimetengwa.
Kuboresha miundombinu ya barabara kwa kujenga
Madaraja/ Makalvati, barabara kwa kiwango cha lami, kufanya matengenezo ya
kawaida ya barabara, muda maalum, maeneo korofi, njia za waenda kwa miguu,
Ujenzi wa Mifereji katika barabara za Manispaa ambapo Jumla ya Tsh 6.2 bilion zimetengwa, Kuboresha
miundo mbinu ya shule za Msingi na Sekondari kwa kununua madawati, kujenga
madarasa, vyoo, nyumba za walimu, maabara na ukarabati wa miundombinu. Jumla ya
Tsh.5.5 billion zimetengwa na Kutoa mikopo kwa wajasiliamali
wa dogo kwa vikundi vya wanawake na vijana ili kuongeza ajira na kukuza kipato
cha Mkazi. Jumla ya Tsh.1.9 billion zimetengwa.
Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kutoa
huduma kwa kujenga Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Tsh.1.7 billion zimetengwa, Kununua magari na mitambo magari
6 ya ofisi, gari moja la maji machafu na gari 1 la maji safi, jenereta. Jumla
ya Tsh 1.35 billion zimetengwa, Kulipa fidia kupisha ujenzi wa
miradi mabali mbali ya maendeleo na kufanya uthamini wa mali za Manispaa. Jumla
ya Tsh.1.2 billion zimetengwa, Kuboresha
usafi wa mazingira na na ukusanyaji taka na
kununua magari makubwa ya taka Jumla ya Tsh.1 billion zimetengwa, Kuboresha upatikana maji safi na salama
kwa wakazi wa Ubungo kwa kujenga na kukarabati miundo mbinu ya maji. Jumla ya Tsh.550 million zimetengwa kwa ajili ya
ujenzi wa miradi ya maji na Mipango miji, kupima na kumilikisha maeneo ya umma
na kutekeleza mfumo wa anuani za makazi (Postcode). Jumla ya Tsh.550 million zimetengwa.
Aidha Halmashauri ya Maninspaa ya ubungo
imetenga Tsh 42 milioni kwa mwaka huu kwa ajili ya kijiji cha michezo kilichopo
kibwegele ambapo kijiji hicho kitakuwa na kiwanja cha mpira wa miguu na viwanja
vya michezo ya watoto, kwa Mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo Tsh 50 milioni zimetengwa,
na Kuboresha na kukarabati masoko Manispaa tumetenga Tsh 1.2 Bilioni, kwa ajili
ya kuboresha masoko ambayo ni Mabibo, Shekilango, Sinza one, na Mbezi pia fedha
hizo zitatumika kulipa fidia na kupima maeneo kwa ajili ya wamachinga na maeneo
ya uwekezaji.
EmoticonEmoticon