Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, wakati wa ziara ya kukagua
udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani humo, huku akiagiza
vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kudhibiti madawa hayo ambayo
yanaharibu nguvu kazi ya Taifa.
Kamishna
wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, akitoa taarifa za
utekelezaji wa zoezi la kudhibiti Dawa za Kulevya Visiwani humo kwa
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto), wakati wa ziara ya naibu waziri kufuatilia utekelezaji wa
zoezi la kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya Visiwani humo.
Mkuu
wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Amani Karume, Fulgenze Mutarasha, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza
kushoto), juu ya hatua zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji na vyombo
vingine vya Ulinzi na Usalama kukabiliana na udhibiti wa uingiaji wa
Dawa za Kulevya kiwanjani hapo.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
Johari Masoud Sururu.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto), akisikiliza jinsi mifumo ya kudhibiti uingiaji haramu
inavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia
Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha.Ziara ya Naibu
Waziri huyo ilikua na lengo la kukagua mifumo inayotumika kudhibiti
uingiaji wa Dawa za Kulevya
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akitoa
maelezo kwa watumishi wa Idara ya uhamiaji waliopo Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya
kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiteta
jambo na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum wakati wa ziara ya
ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya katika Uwanja
wa Ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
EmoticonEmoticon