Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dkt. Ali Mohammed Shein akimsikiliza Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Othman Maalim Othman
(kulia), wakati akitoa maelezo kuhusu majukumu ya Wizara hiyo kwa .
Mwingine ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya
Zanzibar, Mhe. Amina Salum Ali.
Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dkt. Ali Mohammed Shein akipatiwa maelezo ya namna ya wajasiriamali wa
Tanzania watakavyoweza kufaidika kwa kutumia soko la Jumuiya ya Afrika
Mashariki, kutoka kwa Bi. Vivian Rutaihwa, Afisa Biashara kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Naibu
Waziri (OR) wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Khamisi Juma Mwalim anbaye aliwahi kuwa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya
Nje akisaini Kitabu cha wageni katika Banda la Wizara hiyo.
Rais mstaafu wa Awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipatiwa
maelezo ya namna ya wajasiriamali wa Tanzania watakavyoweza kufaidika
kwa kutumia soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka kwa Bi. Vivian
Rutaihwa, Afisa Biashara kutoka Wizara hiyo.
Alhaji Ali Hassan Mwinyi akisaini Kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Silima Haji Kombo, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar naye alitembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje.
Diwani
wa Kata ya Magomeni huko Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa Bw. Tahir
Bakari, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu masuala mbalimbali ya
utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.
Waziri
wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Amina Salum Ali akitoa
hotuba ya kufunga Tamsaha la Tatu la Biashara ambalo ni sehemu ya
shamrashamra ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi.
Mhe. Waziri akikabidhi vyeti kwa baadhi ya washiriki waTamsaha la Tatu la Biashara.
EmoticonEmoticon