Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada
ya kuwasili katika eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi
Mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuanza kwa
ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera. Wengine
katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage, Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Vija Ajira na Wenye Ulemavu Jenista
Mhagama pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiwa
wameshika utepe huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuweka
jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo
hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo
hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo
hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la
mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi
mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la
mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi
mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la
mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi
mkoani Kagera.
Taaswira ya moja ya jengo katika mradi huo wa kituo cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera. PICHA NA IKULU
………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumapili Januari Mosi, 2017
ameendelea na ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kukagua na
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha Kabyaile kilichopo
Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera
Akizungumza na wananchi
waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo hicho cha Afya Rais Dkt
Magufuli amesema serikali kwa sasa imeweka nguvu kubwa katika kurejesha
miundo mbinu ya huduma za jamii iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi
lililotokea Septemba 10,2016 Mkoani humo badala ya kujenga nyumba ya
mwananchi mmoja mmoja.
”Na ndio maana nimeona leo
hapa tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka 2017 niwaeleze ukweli maana kuna
watu wanapitapita huko na wapo wengine nyumba zao zilibomoka kidogo
wakadanganywa wakaambiwa kuwa serikali itakuja kuwajengea nyumba
wakazibomoa zote ”waafwa” kama ulitegemea ukiibomoa utalipwa
fidia,hakuna”
Aidha Dkt Magufuli amemwagiza
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kupeleka huduma ya
umeme katika kituo hicho cha afya alichokiwekea jiwe la msingi,ambapo
pia ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Bilioni moja kwa ajili kutengeneza
barabara inayoelekea kituoni hapo kwa kiwango cha lami.
Pia ameuagiza uongozi wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaojenga kituo hicho cha afya kuharakisha
ujenzi wake na kukamilika kabla ya mwezi februari badala ya Machi mwaka
huu.
Dkt Magufuli ameutaka uongozi na
wananchi wa Wilaya ya Misenyi na maeneo mengine nchini kutumia vyema
mvua chache zinazonyesha mkoani humo kulima mazao yanayokomaa kwa muda
mfupi ili kuepukana na baa la njaa na kwamba serikali haina mpango wa
kugawa chakula cha bure.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
01 Januari, 2017
EmoticonEmoticon