Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ambaye amelazwa
katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es salaam akitibiwa
Januari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe.
Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya
Kairuki akipatiwa matibabu.
Akiwa hospitalini hapo leo
(Jumatatu, Januari 2, 2017), Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya
kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo
kumtakia afya njema Mhe. Ngonyani. Amesema anaamini hivi karibuni
atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kwa upande wake Mbunge huyo
ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini
Dar es Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.
Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.
EmoticonEmoticon