SAME KAYA SACCOS YAWA MKOMBOZI WA WANA -SAME, KILIMANJARO

December 31, 2017

Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) akionyesha moya ya mashine ya kufulia iliyotolewa na Same Kaya Saccos kwa kituo cha afya cha Hedaru, Kilimanjaro.  
Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiwa amenyanyua mikono mara baada ya kukata upete wa kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru, Kilimanjaro.
Watoto yatima na wa mazingira magumu Hedaru wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rosemary Senyamule mara baada ya kupatiwa zawadi ya madaftali.
Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wakati wa hafla hiyo.
Mhe. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Same Kaya Saccos.
Na Mwandishi Wetu.
Same Kaya Saccos  yashika nafasi ya pili Mkoa wa Kilimanjaro 2017 kwa kufanya vizuri katika nyanja zote. Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki hii wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru ambalo ni tawi la 2 ukiacha ofisi ya makao makuu Same. Akizungumza wakati hafla hiyo fupi iliyofanyika Hedaru, Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Bw. Kisimbo alisema kuwa kwa sasa wametimiza miaka 15 na tayari wameshapata tuzo siku ya SACCOS dunia mwezi Oktoba 2017. "Kwa muda ambao tumekuwa tukiwahudumia wanachama wetu tumeweza kupata mafanikio mengi likiwemo la kupata tuzo siku ya SACCOS duniani Mwezi Octoba, 2017," alisema Kisimbo. Kwa upande wake Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule aliwapongeza kwa juhudi ambazo wamekuwa wakizifanya na pia aliwaomba kuendelea kuongeza wanachama wawe wengi zaidi. Mhe. Rosemary Senyamule aliwaomba wanachama waendelee kuwa waaminifu kwa kulipa madeni yao kwa wakati, wananchi wengi kujiunga na SACCOS hiyo iliyoonyesha mfano mzuri wa kutunza fedha za wanachama wake.
RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA FAMILIA TAKATIFU KATIKA KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM.

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA FAMILIA TAKATIFU KATIKA KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM.

December 30, 2017
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.
2.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.
2 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili ya  Familia Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitakiana Heri na Masista walioshiriki katika Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya  Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
WAZIRI NDALICHAKO ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI MAGUFULI ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA LIPA KWA MATOKEO(P4R)

WAZIRI NDALICHAKO ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI MAGUFULI ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA LIPA KWA MATOKEO(P4R)

December 30, 2017
PIC 4
Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia akiwa na viongozi wa Mkoa wa Geita wakati wa kukagua vyumba vya madarasa mwenye miwani kulia ni Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita.
PIC NA.1
Jengo la bwalo la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Magufuli lililopo Kata ya Bwanga Wilayani Chato ambalo limejengwa kupitia mpango wa lipa kulingana na matokeo (P4R).
PIC NA.2
Moja ya bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Magufuli lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 ambalo limetekelezwa kupitia P4R.
PIC NA.3
Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Magufuli, wakwanza kulia ni Mkuu wa shule hiyo na wapili kulia ni Shaban Ntarambe Mkuu wa Wilaya Chato.
PIC NA.5
Mheshimiwa Shaban Ntarambe Mkuu wa Wilaya ya Chato akizungumza na wananchi (awapo kwenye picha) wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu Wilayani Chato.
PIC NA.6
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Magufuli Sekondari.
PIC NA.7
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bwanga wakati wa Ziara yake Magufuli Sekondari.
PIC NA.8
Bwana Exvery Nkanga kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Geita akisoma taarifa ya maendeleo ya elimu Mkoa wa Geita kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia.
…………………………………………………………………………………………………
Na: Magesa Jumapili-Afisa Habari- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Pro.Joyce Ndalichako amefanya ziara fupi Wilayani Chato kwa kuitembelea Shule ya Sekondari Magufuli na kukagua utekelezaji wa miradi ya lipa kulingana na matokeo(P4R) shuleni hapo.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa mabweni, Bwalo, vyoo na vyumba vya madarasa Profesa Joyce Ndalichako ameupongeza Uongozi wa Mkoa, Halmashauri ya Chato na Shule ya Sekondari Magufuli kwa kusimamia vizuri fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kwa ubora na kiwango kinachotakiwa.”Nafurahi kuona fedha za P4R zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kama tulivyokagua na kujionea kiwango kilichojengwa ndio haswa kinachotakiwa ambacho darasa lazima liwe na silling bodi, umeme lakini pia liwe na madirisha tofauti na madarasa tuliyokuwa tunajenga zamani hivyo nawapongeza kwa dhati kabisa viongozi mmefanya kazi kubwa thamani ya fedha inaonekana”.
Profesa Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya tano inajukumu kubwa la kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora katika utoaji wa elimu hivyo miradi ya namna hii inatekelezwa katika Halmashauri nchi nzima. Amesema mwezi desemba 2017 serikali imetoa kwa halmashauri zote shilingi bilioni 15 na milioni 900 za kuendeleza jitihda za kuimarisha miundombinu ya sekta ya elimu ili kuongeza na kuimarisha majengo kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza ambapo zitajenga jumla ya madarasa 415, mabweni 46, matundu ya vyoo 814 na mabwalo 7.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amempongeza Waziri wa elimu kwa kutembelea shule hiyo ili kujionea kazi nzuri iliyofanyika  licha ya kuwa na majukumu mengi ya kitaifa. Amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Geita kwa jitihada zao za kushiriki katika ujenzi wa nyumba vya madarasa 8000  kwa shule za msingi na Sekondari ambapo tangu mkoa uzindue kampeni ya ujenzi huo zaidi ya vyumba 900 vya shule za msingi na zaidi ya 130 vya Sekondari vipo katika hatua tofauti. Amesisitiza kuendelea kuunga mkono jitihada zao kwa kuhakikisha kunakuwa na uwazi katika michango inayotolewa na wananchi.
Mhandisi Robert Gabriel amemhakikishia Waziri wa Elimu kuwa pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi walioandikishwa kujiunda na elimu ya awali, darasa la kwanza na Sekondari hakutakuwa na mwanafunzi atakaye kaa nje ya darasa kwa kuwa jitihada za zinafanyika kwa haraka ili kukabiliana na hali hiyo.
Akiwa katika shule hiyo Mheshimiwa Waziri wa elimu alikagua ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa, matundu 20 ya vyoo, mabweni 2 ya kulala wanafunzi na bwalo  miradi yote hii imetekelezwa na Serikali kupitia mpango wa lipa kulingana na matokeo kwa gharama ya shilingi 570,500,000/=.

WATALII WA NJE NA NDANI WAENDELEA KUMIMINIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

December 30, 2017


Watalii  wakiwasili  uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara uliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Senapa) kwaajili ya kutembelea vivutio vya kitalii wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Watalii wakiwasili uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,kukamilika kwa jengo la wageni wanaowasili na wanaondoka kumerahisisha huduma za usafiri ndani ya hifadhi hiyo.
Afisa Utalii Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa Serengeti mkoa wa Mara,Susuma Kusekwa akizungumza na watalii waliotembelea hifadhi hiyo.
Watalii wakimsikiliza Zacharia Mathayo ambaye ni mwongoza watalii wakati akitoa maelezo kuhusu uhamaji wa wanayamapori aina ya Nyumbu kutoka Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti  hadi Kusini.

Watalii hufurahia kuona wanyama wakubwa wakiwemo Tembo na wengine wanaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Tembo ni mojawapo ya kivutio kikubwa kwa watalii wanaotemebela hifadhi hiyo.
Wanyama wadogo aina ya Pimbi ni sehemu ya vivutio utakavyokutana navyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Wanyama wadogo aina ya Pimbi ni sehemu ya vivutio utakavyokutana navyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imefanikiwa kutangaza vivutio vyake kikamilifu sio kwa watalii wanaotoka  mataifa ya Ulaya,Asia  na Amerika pekee bali pia watalii wa ndani ni sehemu ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
Makundi makubwa ya Simba kama hili utayaona ndani ya hifadhi hiyo.
Serengeti.Idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Senapa) imeongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na sekta ya utalii kukua huku miundombinu ya barabara na viwanja vidogo vya ndege vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo kufanya kazi vizuri.

Afisa Utalii wa Senapa,Evance Magomba alisema kuwa baada ya kujengwa jengo dogo la wageni wanaowasili na wanaoondoka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera idadi ya wageni imeongezeka huku wakala wa makampuni ya ndege wakiweka wawakilishi wao katika uwanja huo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa katika kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu kumekua na safari za ndege 3,724 katika uwanja wa Seronera huku uwanja wa Lobo katika kipindi hicho ni safari 349 na uwanja wa Kogatende safari 564.

Alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna viwanja vidogo vya ndege saba kikiwemo cha  Seronera ambacho ni kikubwa zaidi chenye uwezo wa kupokea ndege  kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 60 ikiwemo ya shirika la Precision Air inayofanya kazi mara nne kwa wiki.

“Miaka miwili iliyopita hatukua na jengo hili la abiria naamini pamoja na sababu nyingine limekua kishawishi kwa wageni kuongezeka kwani linawawezesha kuwa na sehemu nzuri ya kupumzika kabla ya kuanza safari zao,”alisema Magomba

Alisema kutokana na ukubwa wa hifadhi hiyo wanavyo viwanja vingine vilivyosambaa maeneo mbalimbali ili kutoa huduma kwa urahisi na kuwawezesha watalii kupata muda mzuri wa kutembelea vivutio zaidi.

Magomba alivitaja viwanja vingine kuwa ni Kogatenda, Lobo,Ndutu, Kirawira ,Fort Ikoma na Lamai ambavyo hutumika kwa malengo ya kurahisisha kufika eneo husika na kulingana na watalii wanapenda kuona vivutio maalumu.

“Hifadhi ya Serengeti ina uwezo wa kupokea wageni wa aina zote na zipo huduma za malazi zikiwemo hoteli saba,makambi ya kudumu sita na makambi ya muda  zaidi 140 yaliyosambaa na kipekee tuwakaribishe wananchi kutembelea hifadhi zetu kwasababu zipo bei maalumu kwaajili yao,”alisema Magomba

Dereva wa kampuni ya kitalii ya Micato Safaris,Emmanuel Lema alisema huduma za kitaalii nchi zimekua kwa kasi baada ya serikali kupitia Bodi ya Utalii(TTB),shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) na wadau wengine wa utalii kutangaza kwa kiwango kikubwa sekta ya utalii.

Alishauri Tanapa kuongeza ukubwa wa jengo la wanaowasili na kuondoka na huduma zingine muhimu ili kuwawezesha watumiaji wa jengo hilo kupata huduma za kiwango cha juu hasa wakati wa msimu wa utalii.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

DKT MNDOLWA,MAJI MAREFU WAUNGURUMA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA KWAGUDA KOROGWE WAWATAKA WANANCHI KUIPA KURA ZA KISHINDO CCM

December 30, 2017
 Msafara wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa ukitoka Korogwe mjini kuelekea Kata ya Kwagunda Jimbo la Korogwe Vijijini kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za udiwani wa Kata hiyo ambapo Dkt Mndolwa alikuwa mgeni ramsi  gari yaa mbele inayongoza msafara huo ni ya Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
 Msafara wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa ukiwasili eneo la Kijiji cha Mkokola Kata ya Kwagunda ambapo kulifanyika uzinduzi wa kampeni za udiwani wa kata hiyo baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mkokola Kata ya Kwagunda mara baada ya kuwasili kuzindua kampeni za udiwani kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Korogwe Vijijini
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akisaliana na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni hizo mara baada ya kuwasili kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi

 Meza kuu katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akiangalia vikundi vilivyokuwa vikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Korogwe Mjini,Charles Emanuel na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa akiangalia taarifa mbalimbali kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa kampeni hizo
 Sehemu ya wana CCM na wananchi wa Kijiji cha Mkokola wakifuatilia uzinduzi huo aliyevaa shati katika ni Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa wakati wa uzinduzi huo katika ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Korogwe mjini,Charles Emanuel
 Vikundi vya burudani vikiendelea kutoa burudaani wakati wa uzinduzi huo
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa mbele akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakitunza kikundi cha maigizo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini na MNEC na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakitunza kikundi cha maigizo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
 Katibu wa CCM Korogwe mjini,Ally Issa akitunza kikundi cha maigizo katika uizunduzi huo
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa wa tatu kutoka kushoto akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo wa pili ni Mwenyekiti wa CCM Korogwe mjini,Emanuel Charles na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
 Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kushoto akicheza wimbo na Msanii Dkt Njau wakati wa uzunduzi wa kampeni hizo
 Msanii wa Singeli akitumbuiza katika kampeni hizo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi aliwataka kumchangua mgombea wa CCM kwani anafahamu changamoto zao na hivyo itakuwa rahisi kuweza kuzipatia ufumbuzi
Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo akiwataka wananchi kumpa kura za kishindo mgombea wa CCM kama walivyofanya kwenye chaguzi zilizopita ili waweze kushirikiana na viongozi wengine kuwapa maendeleo

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu (MNEC) na Mjumbe wa baraza Kuu la wazazi Taifa  akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumuunga mkono mgombea wa CCM kwa kumpa kura za kishindo
 Mwenyekiti wa CCM Korogwe mjini,Emanuel Charles akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiinguruma katika kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumchangua mgombe wa CCM ili waweze kushirikiana nae kuwapa maendeleo
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiinguruma katika kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumchangua mgombe wa CCM ili waweze kushirikiana nae kuwapa maendeleo
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiinguruma katika kampeni hizo ambapo aliwataka wananchi kumchangua mgombe wa CCM ili waweze kushirikiana nae kuwapa maendeleo
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu (MNEC) na Mjumbe wa baraza Kuu la wazazi Taifa kushoto akimnada mgombea udiwani kata ya Kwagunda
 Diwani wa Kata ya Majengo (CCM) Mustapha akiwasalimia wananchi katika uzinduzi huo
 Msanii Dkt Njau akisailimia wananchi
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa akimnadi Mgombea udiwani wa Kata ya Kwagunda Saidi Shenkawa wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Dkt Edmund Mndolwa kulia akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kushoto wakiondoka eneo la mkutano mara baada ya kumalizika