Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) akionyesha moya ya mashine ya kufulia iliyotolewa na Same Kaya Saccos kwa kituo cha afya cha Hedaru, Kilimanjaro.
Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiwa amenyanyua mikono mara baada ya kukata upete wa kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru, Kilimanjaro.
Watoto yatima na wa mazingira magumu Hedaru wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rosemary Senyamule mara baada ya kupatiwa zawadi ya madaftali.
Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wakati wa hafla hiyo.
Mhe. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Same Kaya Saccos.
Na Mwandishi Wetu.
Same Kaya Saccos yashika nafasi ya pili Mkoa wa Kilimanjaro 2017 kwa kufanya vizuri katika nyanja zote.
Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki hii wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la SACCOS kata ya Hedaru ambalo ni tawi la 2 ukiacha ofisi ya makao makuu Same.
Akizungumza wakati hafla hiyo fupi iliyofanyika Hedaru, Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Bw. Kisimbo alisema kuwa kwa sasa wametimiza miaka 15 na tayari wameshapata tuzo siku ya SACCOS dunia mwezi Oktoba 2017.
"Kwa muda ambao tumekuwa tukiwahudumia wanachama wetu tumeweza kupata mafanikio mengi likiwemo la kupata tuzo siku ya SACCOS duniani Mwezi Octoba, 2017," alisema Kisimbo.
Kwa upande wake Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule aliwapongeza kwa juhudi ambazo wamekuwa wakizifanya na pia aliwaomba kuendelea kuongeza wanachama wawe wengi zaidi.
Mhe. Rosemary Senyamule aliwaomba wanachama waendelee kuwa waaminifu kwa kulipa madeni yao kwa wakati, wananchi wengi kujiunga na SACCOS hiyo iliyoonyesha mfano mzuri wa kutunza fedha za wanachama wake.