Na: Frank Shija – MAELEZO.
MAKOMANDOO
wa Jeshi la Ulinzi wanatarajiwa kupamba sherehe za maadhimisho ya miaka
55 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo wwatacheza gwaride la kimyakimya.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge,
Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama kupitia
taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Jenista amesema kuwa mbali
na maonyesho hayo pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi
vya Bendi ya Muziki wa kizazi kipya na Kizazi cha zamani, ngoma za asili
za mikoa ya Mbeya, Pwani, Lindi na kimoja kutoka Zanzibar.
Waziri
Mhagama ameongeza kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha ametoa wito
kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika
viwanja vya Uhuru siku hiyo ya tarehe 9 Desemba ili kusjumuika na
Watanzania wote katika kuadhimisha sherehe hizo.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu”
EmoticonEmoticon