Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa
Shirikisho la Mpira Brazil (CBF), kutokana na vifo vya wachezaji wa timu
ya soka Chapecoense Real ya Brazil.
Rais wa TFF Malinzi, katika salamu za
rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Brazil (CBF), Lucca
Victorelli amesema ajali hiyo iliyoua watu wengi ni tukio la
kusikitisha kwenye familia ya soka duniani na limetokea katika kipindi
kigumu.
EmoticonEmoticon