Bukoba, Novemba
29, 2016-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)
leo imetoa msaada mifuko ya saruji 500 yenye thamani ya shilingi
milioni 10 kwa wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotoa mkoani Kagera.
Msaada huo ni kuitikia wito wa serikali kwa mashirika, watu
binafsi na watu wenye mapenzi mema wa kujitoa kusaidia wahanga wa
tukio hilo.
Akizungumza
katika tukio la kukabidhi msaada huo katika Ofisi ya Mkuuu wa Mkoa wa Kagera
mjini Bukoba, Meneja Usalama wa SBL, Sebastian Kalugulu aliwapa
pole wahanga wa tetemeko hilo kwa kuwahakikishia kwamba
SBL kila mara iko tayari kusaidia pindi inapohitajiwa na
jamii.
“”Tunatoa
pole ya dhati na masikitiko yetu kwa wahanga wa tetemeko la
ardhi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka,” alisema Kalugulu,
na kuongeza kwamba SBL inaungana na watu wengine wenye mapenzi mema
kutoa msaada wa kibinadamu kwa ajili ya kuwasaidia kuhimili kadhia
iliyowapata na kurudi katika shughuli zao kawaida.
Kalugulu
alithibitisha tena kwamba kampuni hiyo ya bia imejikita katika
kuunga mkono serikali na watu binafsi wenye mapenzi mema,
mashirika na makampuni katika kuisaidia jamii katika
maeneo SBL inapoendesha shughuli zake.
“Ni
matumaini yetu kwamba msaada huu utachangia katika
michango iliyokwishatolewa na wasamaria wengine na kwamba
itawawezesha wahanga hao kujenga miundombinu
iliyoharibika na hata kuboresha maisha yao.”
Akizungumzia
mchango uliotolewa na SBL, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum
Kijuu alisema kwamba msaada huo unachangia katika
michango mingine kutoka kwa watu wenye mapenzi
mema kutoka ndani, mikoani na kimataifa ambao kmwa
ukarimu waliitikia wito wa serikali wa kusaidia.
Mkuu huyo wa mkoa
alisema kuwa atahakikisha kuwa msaada huo unaenda kwenye lengo
lililokusudiwa na kutoa wito kwa watu
zaidi kuendelea kuwasaidia wahanga.
EmoticonEmoticon