WATANZANIA takribani asilimia 40 wanatakiwa wawe wamejiingiza kwenye uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020 ili kuweza kusaidia kukuza ajira za vijana na kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla.
Akizungumza
hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya
kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage amesema kuwa Serikali
imeazimia kufikisha asilimia 40 ya watanzania kufanya shughuli za
uchumi wa viwanda kufikia 2020.
“Tunataka
mpaka kufikia 2020 watanzania takribani asilimia 40 wawe wamejikita
kwenye uchumi wa viwanda ili kusaidia kukuza ajira kwa vijana na
kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii nan
chi yetu kwa ujumla” alisema Waziri Mwijage.
Aidha
Waziri Mwijage amesema kuwa Uchumi wa viwanda unatakiwa kukua nchini
kuwezesha kuzalisha bidhaa bora zitakazouzwa ndani na nje ya nchi ili
kukusanya kodi kwa ajili ya kupata huduma bora za kijamii kwa maendeleo
ya wananchi wa Tanzania .
Kwa
upande wa Afisa Mkuu wa elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Nchini (TRA) ambao ni wadhamini wa mkutano huo Bi. Rose Mahendeka
alisema kuwa wafanya biashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa
kuuza bidhaa kwa kuweka msimbomilia(Barcode) wanapaswa kupitia TRA kwa
ajili ya usajili na uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN)
kabla ya kwenda kupata huduma ya msimbomilia.
“Wafanya
biashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka
msimbomilia(Barcode) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na
uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN) kabla ya kwenda
kupata huduma” alisisitiza Bi. Mahendeka. Aidha Bi.
Mahendeka
alisema kuwa wafanya biashara ambao wanahitaji kuuza bidhaa zao kwa
kutumia msimbomilia wanapasa kulipa kodi bila ya kukwepa ili kuwezesha
Tanzania kupiga hatua kufikia uchumi wa viwanda ili kupata huduma bora
kwa maendeleo ya jamii.
Naye
Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara amesema kuwa
wafanyabiashara wanatakiwa kutumia msimbomilia wa Tanzania ili kuweza
kutangaza bidhaa za nchini ili kuweza kupata soko la kimataifa na
kufikia uchumi wa kati .
“Ni
lazima kutumia msimbomilia wa Tanzania kwa kila mfanyabiashara na
mjasiriamali ili kuweza kutangaza bidhaa za nchini ili kuweza kupata
soko la kimataifa na kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda vikubwa na
vidogo” alisema Bw. Mazara.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage akiongea na wadau
mbalimbali wa biashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kutumia
msimbomilia(barcode) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia
(Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage wa pili kulia
akikata keki kuadhimisha mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali
inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es
salaam wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kulia akimpa
mkono wa pongezi Afisa Mkuu wa elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya
Mapato Nchini (TRA) kwa kudhamini mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi
isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1)
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kushoto akipokea
zawadi kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Shea illushion kulia wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali
inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es
salaam. Na Mpiga picha Wetu . Dar es salaam.
EmoticonEmoticon