SINGIDA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS LA USAFI WA MAZINGIRA KIKAMILIFU

November 26, 2016

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na wananchi wa Mji wa Singida wakikusanya uchafu katika siku ya Usafi Kitaifa Mjini Singida.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipeleka uchafu katika kizimba cha uchafu cha soko  kuu la Singida lililoko katika Mtaa wa Ipembe
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiandaa mche wa mti kitalamu kabla ya kuupanda katika zoezi la usafi na upandaji miti mjini Singida leo.
Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina Akipanda Mti aina ya Mparachichi katika eneo la Misuna Stand Mpya Mjini Singida leo katika Zezi la usafi wa mazingira Kitaifa. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)

 Na Evelyn Mkokoi – Singida
Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.
Akishiriki zoezi hilo  Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana  singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoeZi hilo.
Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.
“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.
Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »