Dar es Salaam, 21st October 2016 – Taasisi inayoongoza Tanzania kwa kubobea katika kutoa mikopo nafuu, Bayport Financial Services katika kipindi cha miaka 10 iliyopita imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuboresha maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia utoaji wa mikopo.
Bayport Tanzania ni miongoni mwa taasisi tanzu kumi za Taasisi ya Bayport Group ambayo hutoa ufumbuzi wa kifedha kwa watu binafsi walioko katika ajira rasmi au waliojiajiri ndani ya soko linaloibukia. Huduma zinazotolewa na taasisi hiyo zinaboresha ujumuishwaji kifedha kwa watu ambao hawana uwezo wa kuzifikia huduma za kawaida za kibenki au walio na kiasi kidogo cha fedha katika benki.
Baada ya kuanza shughuli zake nchini Zambia mwaka 2001, shughuli za Bayport kwa hivi sasa zinaendeshwa katika nchi saba barani Afrika na nchi mbili ndani ya Amerika Kusini. Nchi hizo ni Zambia, Uganda, Ghana, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Msumbiji, Colombia, na Mexico.
Hivi sasa Bayport imekuwa ni msingi wa kuaminiwa na mteja ikiwa na takribani wateja 518,000 ambao kila mara wamekuwa wakipata na hata na kufurahia huduma inazozitoa.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, Bayport imeshatoa zaidi ya shilingi bilioni 48 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015 peke yake. Kwa upande mwingine Bayport inachukuliwa kuwa ni ‘mlipa kodi mkubwa’ nchini Tanzania ikiwa imelipa zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka wa fedha 2014.
“Matamanio yetu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwapa fursa ambazo zitawanufaisha sio wao peke yao bali pia watoto wao na kizazi kijacho,” alisema Mbaga katika mazungumzo yake na wanandishi wa habari hivi karibuni.
Aliongeza, “Tunawasaidia kwa kuangalia unafuu utakaotokana na mtiririko wa fedha katika kipindi kifupi ambapo matokeo yake husaidia familia katika kuongeza na kuwa na ustawi wa kifedha wa kudumu.”
Bayport Tanzania ilianzishwa mwaka 2006, na kwa haraka imekuwa ni mtoaji wa mikopo kwa wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi. Kuwepo kwa ofisi zake 83 za kudumu na matawi 45 ya muda kumeifanya kufika kila mkoa kwa Tanzania Bara.
Kampuni hii ina wafanyakazi wa kudumu 300 na mtandao wa mawakala wa mauzo zaidi ya 1000.
“Kazi ambazo tumekuwa tunazitoa zimechangia kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini,” anasema Mbaga.
Kwa mujibu wa utafiti wa Ujumuishaji wa Nguvu Kazi (Integrated Labour Force Survey 2014), kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tanzania kilikuwa ni asilimia 13.7.
Mbali na kutoa mikopo, mambo mengine ambayo Bayport inajishughulisha nayo ni pamoja na bidhaa za bima kama vile Sera ya Ulinzi Kielimu ambayo inashughulikia utegemezi wa ada katika elimu kwa muda wa hadi miaka mitatu katika iwapo kwa bahati mbaya mwenye bima hiyo atafariki. Sera ya Bima ya Maisha ya Bayport inahusisha kulipia salio lililobakia iwapo wateja watapunguzwa kazi, watakuwa wamepata ulemavu, watafariki au kupatwa na maradhi kama vile saratani.
Hivi karibuni Bayport ilizindua aina ya mikopo kwa ajili ya nyumba ambayo inawawezesha wateja kumiliki kiwanja kilichopimwa. Bidhaa hiyo inawezesha Bayport kuifikisha mikopo yake kwa mkopaji kwa kutumia kiwanja kilichopimwa kama dhamana.
Akizungumza kuhusu sera ya Bayport kuhusu kuwajibika kwa huduma za kijamii, Mbaga alisema kwamba elimu ndio kipaumbele chake. “Kupitia mkakati wa ‘Badilisha Maisha’ tumeshafanya ukarabati wa madarasa katika shule kadhaa, kutoa msaada wa madawati, kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na kutoa msaada wa vitabu. Tangu mwaka 2006, tumetoa misaada ya moja kwa moja kwa wanafunzi 1,500 wa shule za msingi na sekondari.”
Bayport pia inawasaidia watoto yatima. Mradi wa mfano unajidhihirisha kwa kuisaidia shule ya watoto yatima inayodhaminiwa na Mfuko wa Fursa kwa Wote (EOTF) ambapo Bayport imeboresha shule hyo ya awali kuwa katika viwango vya kisiasa.
Uwekezaji wa shilingi milioni 200 uliofanywa na Bayport umewezesha kuwepo kwa mazingira rafiki ukiwepo mwanga wa asili na sehemu asilia za kupitisha hewa kwa ajili ya watoto 40 wanaohudumiwa akatika kituo cha EOTF na wengine 60 kutoka katika vijiji jirani wakinufaika.
Akiangazia kuhusu safari ya miaka kumi ya mafanikio katika biashara hapa nchini, Mbaga anasema kwamba Kampuni hiyo inajivunia kukua kwake na kukomaa ambako imeweza kufikia katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita. “Tunasherehekea fursa hii na uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha ya wateja wetu, wadau, wafanyakazi na jumuia katika maeneo tunakoendesha shughuli zetu.”
Alidokeza kuwa dira ya kimkakati ya taasisi hiyo na utekelezaji wake uliokwishafanyika umejikuta ukipata msaada kutoka kwa wawekezaji, miongoni mwao ni kampuni ya uwekezaji wa Sweden ya AB Kinnevik. Julai 2010 kampuni hiyo iliwekeza dola milioni 40 katika Bayport Group na hivyo kuwa taasisi pekee yenye hisa nyingi ndani ya Bayport.
Miezi minne baadaye Bayport ilitoa kwa mara ya kwanza katika masoko ya madeni ya mitaji kimataifa kwa kukusanya jumla ya dola milioni 100.
“Mwaka 2016 uongozi wa Bayport uilifikia dola milioni 250 ikiwa ni uwezo wa salio kubwa kupatikana kutoka Shirika la Uwekezaji Binafsi Ng’ambo (Overseas Private Investment Corporation-OPIC), ambayo ni taasisi ya maendeleo ya fedha ya serikali ya Marekani. Mkopo huo wa muda mrefu utasaidia ujumuishwaji wa kifedha wa taasisi na ajenda yake ya kukua katika shughuli zake zote. Kama taasisi tanzu ya Bayport, Bayport Tanzania inachangia katika historia ya uwekezaji wa taasisi na faida zinazotoka ndani yake.”
Kwa mujibu wa Mbaga mkakati wa kibiashara wa Bayport upo katika mabadiliko ya bidhaa na ubunifu wa kiteknolojia na ‘watu wakiwa ndio nguzo yetu kuu’.
Ndani ya mkakati huo wa taasisi, Bayport Tanzania mwaka 2015 utambulisho wake ulipata chapa mpya ikiwa na ujumbe uliojikita kwa watu, na hivyo kuipa taasisi fursa ya ya kujiweka tena yenyewe katika mtoaji wa ufumbuzi wa kifedha.
“Bidhaa yetu mpya haikuanzishwa katika hali ya upweke. Iliibuka ndani ya falsafa yetu ya kibiashara ambayo inaitwa ‘The Bayport Way”, Mbaga alifafanua na kuongeza, “Falsafa hiyo inahusu mambo yote ya namna tunamchukulia mteja, awe ni mwajiriwa, mteja au mwekezaji, na jinsi ambavyo tunaongeza thamani katika maisha yao.”
Kama taasisi Bayport inaamini kwamba mikopo ni nyenzo yenye nguvu inapotumiwa kistaarabu na katika mazingira yaliyo na ufanisi. “Hakuna kinachotufanya kama pale ambapo tunapowaona wateja wetu wakiitumia mikopo katika matumizi chanya na kuendesha shughuli za kiuchumi ambazo kimsingi zinaboresha maisha yao,” Mbaga alisema.
Ofisa Mtendaji Mkuu huyo aliwashukuru wateja wa Bayport Tanzania, wafadhili, serikali na wadau wengine kwa kuiunga mkono taasisi hiyo bila kuchoka katika kipindi chote cha miaka kumi.
Alisema, “Imekuwa ni safari ya kuvutia iliyojaa mafanikio. Bila wadau wetu hawa hatungaweza kufikia hatua hiii. Nawahakikishia kwamba Bayport Tanzania inaimarika kila mwaka. Wakati tunaelekea katika mwongo mwingine tumejipanga na tumejikita katika kufanikiwa hata katika viwango vya hali ya juu vya ufanisi katika kutoa kutoa bidhaa zisizo na ushindani nchini Tanzania.”
EmoticonEmoticon