Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) akitoa maelekezo ya
kiutendaji kwa Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko
Ngoroma (kushoto) alipotembelea kituo hicho, kulia ni Mhasibu wa TEMESA
Tanga Bw. Lusenga David.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto aliyesimama) akizungumza
na watumishi wa TEMESA Tanga wakati alipotembelea kituo hicho kuangalia
hali ya utendaji kazi, kulia ni Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi
Mahangaiko Ngoroma.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Tanga
……………………………………………….
Na Theresia Mwami TEMESA TANGA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka wafanyakazi wa kivuko cha
Mv Tanga kuzingatia usalama wa abiria kwa kufata kanuni na Sheria za
usafirishaji wa abiria kupitia vivuko.
Amesema hayo alipotembelea na
kuongea na watumishi wa kivuko cha MV. Tanga kinachosafiri kati ya
Pangani na Bweni na kuwasisitiza watumishi hao juu ya suala la usalama
wa abiria na kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa mapato ya kivuko
hicho.
Ndugu zangu hapa tunabeba roho za
watanzania wenzetu tuwe makini sana na kuzingatia Sheria na taratibu
zilizopo ili kuhakikisha usalama wa hawa abiria tunaowahudumia”
Alisisitiza Dkt Mgwatu.
Kwa upande wake Meneja Msaidizi
TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma amemuahakikishaia Mtendaji
Mkuu kuwa watazingatia taratibu na Sheria zilizopo ili kuhakikaisha
usalama wa abiria wanaowahudumi kupitia kivuko cha Mv Tanga na vivuko
vingine vilivyopo mkoani Tanga.
Aidha kwa upande wao watumishi wa
Mv Tanga wamemwaomba Mtendaji Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto
mbalimbali zilizopo zikiwepo uhaba wa vifaa kwa ajili ya kutekeleza
majukumu yao ya kila siku.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt.
Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo
kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto
zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huyo.
EmoticonEmoticon