Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akifanya mahojiano ya kipindi maalum cha heloo
Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio Uhuru FM cha Jijini Dar
es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo
Jijini humo. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho, Sheila Simba.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa kipindi
cha heloo Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Uhuru FM,
Sheila Simba wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini
humo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akibadlishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Angel
Akilimali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo ya ziara yake ya kutembelea
vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akizungumza na wahariri na waandishi
wa gazeti la Uhuru wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari
leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Gazeti
hilo, Ramdhani Mkoma na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara
Habari( MAELEZO), Jonas Kamaleki.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa habari za
michezo wa gazeti la uhuru, Sophia Ashery wakati wa ziara yake ya
kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa gazeti la
uhuru, Njumai Ngota wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari
leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru, Ramadhani Mkoma akimpatia maelezo
kuhusu uhifadhi wa magazeti ya zamani kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wahariri wa Gazeti la Uhuru wakifuatilia kwa makini mkutano wa
mazungumzo baina yao na Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa
ziara yake ya kutembelea ofisi za gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akizungumza wakati wa mkutano wake na bodi ya
uhariri wa gazeti la uhuru wakati wa ziara yake ya kutembela ofisi za
gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mhariri
wa Picha, Yassin Kayombo na Mhariri wa Habari Abdallah Kimweri.
Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas akisalamiana na Mhariri msanifu kurasa wa
gazeti la Uhuru, Jane Mihanji mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na
Bodi ya Uhariri ya gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.
………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO.
Dar es Salaam.
SERIKALI
imesema muswada wa sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo
vya habari kuiomba radhi jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari
zenye upotoshaji na hawatochukuliwa hatua za kisheria kutoka katika
mamlaka zinazohusika.
Akizungumza
katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar
es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya
waandishi wa habari kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake
wausome na kuelewa na kisha watoe maoni yao ili kuuboresha zaidi.
“Sifa
moja ya taaluma ya habari ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa
kwa mwanahabari kukanusha na kueleza ulichokosea hivyo mwandishi
hatashtakiwa endepo akiona amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba radhi”
alifafanua Mkurugenzi Abbas.
Kwa
mujibu wa Abbas alisema kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala
ya maadili kwa waandishi wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa
waandishi hao kuhojiwa na kutoa ufafanuzi wa jambo husika.
Aidha
Abbas alisema kuwa ipo misingi ya haki ya habari iliyoanishwa katika
mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 cha mkataba wa geneva wa
mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo
ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.
Aidha
Abbas aliongeza kuwa muswada huo umelenga kulinda maslahi na usalama wa
wanahabari kwani unazungumzia hali halisi ya mwandishi wa habari
ukilinganisha na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 inayozungumzia haki ya
chombo cha habari pekee.
Mkurugenzi
Abbas alisema kila taaluma duniani ina bodi yake hivyo imefika wakati
kwa Tanzania napo kuwa na bodi ya wanahabari ili kuweza kuitendea haki
taaluma ya habari.
EmoticonEmoticon