Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk.
Juliana Pallangyo (kushoto) akifugua kongamano la nne linalohusu gesi
na mafuta lililoambatana na maonesho , lililokutanisha wadau mbalimbali
kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi,
vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk.
Juliana Pallangyo (kushoto), akibadilishana mawazo na Kaimu Kamishna wa
Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile (kulia) katika
kongamano hilo
Kutoka
kulia; mwakilishi kutoka Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa
Abraham Temu, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James
Andilile na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kongamano hilo.
Washiriki
kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na
gesi, vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali wakifuatilia hotuba
iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika
kongamano hilo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya
Musomba (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo
(kulia) kwa mchango wa shirika hilo katika kufanikisha kongamano hilo.
Mwakilishi
kutoka Benki ya Standard Chartered, Thomas Bisonga (kushoto) akipokea
tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa
benki hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Mwakilishi
kutoka kampuni inayojihusisha na ujenzi wa mabomba ya gesi kutoka China
(kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo
(kulia) kwa mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Meneja
Mawasiliano kutoka kampuni ya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta
nchini ya Statoil, Genevieve Kasanga (kushoto), akipokea tuzo kutoka
kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa kampuni hiyo
katika kufanikisha kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba akieleza jambo katika kongamano hilo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk.
Juliana Pallangyo (katikati waliokaa mbele) akiwa katika picha ya
pamoja na sehemu ya washiriki wa kongamano hilo.
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Kongamano
la Nne linalohusu sekta ndogo ya mafuta na gesi lililoambatana na
maonesho kuhusu sekta hiyo na kukutanisha Wadau mbalimbali ikiwemo
Kampuni zinazojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi,
Vyuo Vikuu, Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali limeanza kufanyika
jijini Dar es Saalaam.
Kongamano
hilo lilifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo ambapo aliwaeleza wadau
hao kuwa, usimamizi madhubuti wa sekta ndogo ya gesi na mafuta utaleta
mapinduzi makubwa kwenye ukuaji wa viwanda na kuiwezesha Tanzania
kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Katika
kongamano hilo linalofanyika kuanzia tarehe 20 – 21 Oktoba, 2016, Dk.
Pallangyo alisema kuwa kutokana na kiasi kikubwa cha gesi
kilichogunduliwa ambacho ni futi za ujazo trilioni 57.2, kampuni
mbalimbali za kigeni zimeanza kujitokeza na kuwekeza katika mikoa ya
Lindi na Mtwara ambapo gesi imegunduliwa
Alisema
kutokana na uwekezaji katika shughuli za gesi na mafuta, kumekuwepo na
mabadiliko ya kiuchumi katika mikoa hiyo kama vile kuongezeka kwa fursa
za ajira, malazi na utoaji wa huduma kwa wawekezaji.
Aliongeza
kuwa ni vyema wananchi hususan wa maeneo hayo kujiandaa na uwekezaji
mkubwa katika mikoa hiyo ambapo kwa sasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara
kunatarajiwa kujengwa viwanda vikubwa vya mbolea, vitakavyoleta neema
katika mikoa hiyo.
Alisema
katika kujiandaa na kasi ya ukuaji wa sekta za gesi na mafuta nchini
serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
kunakuwepo na sera na sheria zitakazowezesha wazawa kuwa sehemu ya
umiliki wa uchumi wa gesi na mafuta.
Alitaja
mikakati mingine ni pamoja na uanzishwaji wa kozi zinazohusu masuala ya
gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM).
Aliongeza
kuwa, Serikali imekuwa ikipeleka nje ya nchi kusomea masuala ya gesi na
mafuta katika ngazi ya shahada ya uzamili (masters degree), wanafunzi
wanaofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi katika ngazi ya shahada.
“Lengo
letu kama Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalam wa
kutosha watakaoshiriki katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa
kwenye makampuni yanayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi na
mafuta,” alisema Dk. Pallangyo.
Wakati
huo huo akizungumza katika kongamano hilo, mwakilishi kutoka Taasisi ya
Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu alisema kuwa lengo la
kongamano hilo lilikuwa ni kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu sekta
za gesi na mafuta nchini.
Alisema
mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na uelewa kuhusu
sekta za gesi na mafuta, sera na sheria za mafuta na gesi,
ushirikishwaji wa wazawa kwenye sekta za gesi na mafuta, changamoto na
matumizi endelevu ya mafuta na gesi na rushwa.
Kongamano
hilo liliandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na
Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji
(EWURA) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
EmoticonEmoticon