KUFUATIA Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari
ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba
Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu.
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni,
Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya
Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana
Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea
chini kutoisha.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa
Wilaya, Thobias Mwailapwa, amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement) na kuyataka mashirika na
taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya wanafunzi kusomea
chini.
Kwa upande wake Afisa elimu shule ya msingi jiji , Khalifa
Shemahonge, amesema madawati hayo yatatumika kama inavyokusudiwa na kuahidi
kuyatunza ili kuongeza uelewa wa wanafunzi
darasani.
Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement
(Simba Cement), Dianna Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga,
Thobias Mwailapwa, madawati 100 kwa shule tatu za msingi, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba za halmashauri ya jiji la Tanga kupunguza
uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa,
akimkabidhi Afisa Elimu Shule ya Msingi halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa
Shemahonge madawati 100 kwa shule tatu ya, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba yaliyotolewa na
kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi kupunguza uhaba wa madawati kwa shule
hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa mwenye suti bluu (katikati)
na Afisa Elimu shule ya msingui halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa
Shemahonge (kulia) wakiwa na wafanyakazi wa kiwanda cha Simba Cement
mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule tatu za halmashauri
ya jiji la Tanga .
Walimu wa shule za msingi Magaoni, Kiruku, Martin Shamba na Mkombozi
wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga na wafanyakazi
wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya
madawati 100 kwa shule hizo.
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929
EmoticonEmoticon