Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazngira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na maafisa na
waaandishi wa habari alotangulizana nao katika DAMPO la mji wa Tabora na
kushangazwa na hali halisi ya DAMPO hiyo na taarifa ya mazingira
aliyopewa na mkoa kuhusu usafi wa mazingira wa mji wa Tabora
Bw. Benjamini Dotto Afisa
Mazingira kutoka Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira
NEMC (katikati) akieleza kitaalam nini kifanyike katika DAMPO la Mji wa
Tabora kabla ya manispaa kuwasilisha mpango mkakati kuhusu dampo la mji
huo. (Picha na Evelyn Mkokoi)
…………………………………………………………
EVELYN MKOKOI-TABORA
Kupitia Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameipa adhabu Halmashauri
ya Maispaa ya Mji wa Tabora kwa kuitoza faini ya shilingi Milioni kumi
na mbili na kutakiwa kulipa faini hiyo kwa muda wa wiki mbili, kwa kile
kilichodaiwa ni kutokutii mamlaka za juu na kusema uwongo kuhusu hali ya
usafi wa maingira ya mji wa Tabora.
Alipokoukuwa katika siku ya Pili
ya ziara yake mkoani Tabora baada ya kupata taarifa ya hali ya mazingira
ya mkoa huo, Na kuambiwa kuwa ni ya kuridhisha na kuwa DAMPO la mji huo
ambalo siyo rasmi,lipo katika hali ya kuridhisha ndipo alipoamua
kjutembelea DAMPO hilo na kujioea hali ya uchafu isiyovumilika kwa taka
ngumu na hatarishi, kutomwagwa katika eneo husika na kuzagaaa
barababarani.
Aidha kufuatia malalamiko ya
wakazi wa mji huo, Mpina halikadhalika aliktembelea soko ya mji wa
Tabora na kushuhudia Dampo katikati ya soko hilo lenye taka mbichi zenye
harufu kali ambayo huweza kuhatarisha maisha ya watumiaji wa soko hilo
kwa kupata magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa
Manispaa ya Tabora Bw. Bosco Nduguru alisema ofisi yake ilikuwa na
mpango wa kuhamishia soko hilo sehemu nyingine na kukubali changamoto
zilijitokeza sokoni hapo na kuzifanyia kazi wakati mwenyekiti wa soko
hilo bwana Bakari Mpumila alieleza kuwa kuhamishwa kwa soko hilo
hakuwezi kuwa suluhisho la kudumu kutatua changamoto za usafi wa
mazingira kwani dampo linalotumika katikati ya soko hilo limekuwa ni
kero iliyoshindikana toka kwa uongozi uliopita na Kumshukuru Naibu
Waziri Mpina kwa ziara yake kwani ana imani kuwa sasa kero hiyo
imeshatapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Pamoja na kulipa faini hiyo
manispaa pia inatakiwa kuondosha taka hizo a kumwaga kifisi cha molamu
katika eneo hilo na kurekebisha mazingira ya choo sokoni hapo.