Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo
shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam
zilifanyika.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba
akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti
iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa
Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es
Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini
Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya
kilwa wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga
na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure
kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
....................................................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Oktoba 2016 ameongoza mamia ya wakazi wa
mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti
inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.
Akihutubia
mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya
Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es
Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe
vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa
inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora
katika utunzaji wa Manzingira.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini
Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa
asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.
Amesema kuwa
jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia
katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari
za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Makamu wa
Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa
ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi
kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za
kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza
jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji
wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti
iliyopandwa.
Amesema anafaraja
na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa
endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio
na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.
Baada ya
kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba
na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya
kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan
Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi
walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.
EmoticonEmoticon