Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi
akizungumza wakati wa kufungua rasmi Matembezi ya Hisani kwa ajili ya
kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo
Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika
viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi
1,502,680,000/= zilichangwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga akizungumza
na washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa
Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam.
Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la
Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/=
zilichangwa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi
akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza Matembezi ya Hisani kwa
ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera”
leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga, Mwenyekiti wa
Wabunge kutoka Kagera, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko
lililotokea mkoani Kagera iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu
na Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na
Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/=
kilipatikana.
Naibu Waziri wa Nchi, OWM –Sera,
Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi
akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea
mkoani Kagera iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo
Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisania
ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi
akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirkiano wa Afrika Mashariki katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya
“Walk for Kagera” Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Aziz Mlima leo
Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi
akishiriki Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa
Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam.
Katika matembezi hayo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kimepatikana.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya
kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera iliyoandaliwa
na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa
kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio katika
hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na
Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/=
zilipatikana.
Wawakilishi wa Jumuiya ya Wabohora
nchini wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi
yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia wahanga
wa Tetemeko Mkoani Kagera kwa Rasi wakati wa Matembezi ya hisani
yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii wa PPF Bw. William Erio na Afisa Uhusiano wa PPF, Lulu
Mengele wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi
yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa
Tetemeko Mkoani Kagera wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Waziri wa Mmbo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi
akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirkiano wa Afrika Mashari katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya “
Walk for Kagera” Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Busemaker
akipokea cheti kwa ajili ya kutambua udhamini wa Benki hiyo katika
kufanyikisha matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa
Tetemeko la Kagera leo Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi
akiagana na baadhi ya washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya
kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo
Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika
viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi
1,502,680,000/= zimechangwa.
……………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, MAELEZO
TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5
zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for
Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia
wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu
mjini Bukoba Mkoani Kagera.
Akizungumza mara baada ya
matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi
aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo
ya hisani.
“Nawapongeza sana wadau wote
mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa
umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii
inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera
kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko
hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.
Balozi Kijazi aliongeza kuwa
kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake
imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja
ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.
“Najua kuna athari kubwa imetokea
kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada
kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote
katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.
Awali akisoma maelezo ya tathmini
ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –
Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi
amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba
zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo
44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.
Kwa upande wake Kiongozi wa
Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo
na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada
wao.
Matembezi hayo ya hisani kwa ajili
ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi
yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.
EmoticonEmoticon