Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 6 kutoka kwa
mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw. Deo Senya wakati Jumuiya ya
Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) walipofanya Harambee ya kuchangia
wahanga wa Tetemeko la Ardhi kule Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa
wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo, Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya
ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wafanya Biashara Kariakoo Bw.Philimin Lomano Chonde.
Katika harambee hiyo jumla ya
shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu zilikusanywa na vitu
mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 31564800/= jumla ya
michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/= harambee hiyo leo
ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea mpaka siku ya jumamosi
ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi na wafanyabiashara
mbalimbali wametakiwakuendelea kuchangia kwa kupitia jumuiya yao ya
wafanyabiashara mpaka siku ya jumamosi.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema akipokeamsaada wa viatu kutoka kwa wafanyabiashara wa kikundi cha
Raha Square wafanyabiashara ambao wametoa mchango ubwa sana wa fedha na
vitu mbalimbali katika harambee hiyo.
Wafanyabiashara wa Raha Square Kariakoo wakikabidhi mcahngo wao wa fedha kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
Raha Square wakikabidhi Magodoro , Nguo, Vikoi , Mashuka na vitu vingine mbalimbali katika harambee hiyo.
Wakikabidhi Suti na vitengi pamoja na mashuka katika harambee hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ilala akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo mara baada ya harambee hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema akiwahutubia wafanyabiashara na wananchi mbalimbali waliohudhuria
katika harambee hiyo.
Mfanyabiashara Mohammed Abdallah
Nofa akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wake wa shilingi
500.000 kwa Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema wa pili kutoka kulia .
katika picha kulia ni Edward Mpogolo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala
na Kushoto ni Katibu wa JWK Bw. Abdallah Mwinyi
Wafanyabiashara kutoka Raha Square wakikusanya michango yao ya fedha taslimu na vifaa mbalimbali kabla ya kuvikabidhi leo.
Kiongozi wa Wafanyabiashara wauza
Simu za mkononi Bw.Stanley Mwakipesile akizungumza machache mara baada
ya kukabidhi mchango wao zaidi shilingi milioni 1.500.000 kwa mkuu wa
wilaya ya Ilala katika Harambee hiyo.
EmoticonEmoticon