Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokea kiasi cha Shilingi Milioni
1.6 kutoka kwa Mratibu Taifa wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Bi. Mariam Kilembe wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu, kwa ajili ya Kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera, leo Bungeni Mjini Dodoma.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amepokea msaada wa sh. milioni 121.679 ili kusaidia wananchi
waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Jumamosi,
Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.
Msaada huo umetolewa leo (Ijumaa,
Septemba 16, 2016) na wadau mbalimbali wakiwemo Meneja Rasilimali Watu
wa Kampuni ya Caspian, Bw. Omid Karambech aliyetoa sh. milioni 100.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Bordar Limited, Bw. Wu Yahui aliyetoa sh. milioni 20 pamoja
na Bi. Mariam Kitembe aliyetoa sh. milioni 1.679 kwa niaba ya Wauguzi
walioshiriki mafunzo ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi kutoka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Akipokea msaada huo katika viwanja
vya Bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu amewashukuru kwa michango yao ya
fedha na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia
watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi
kutokea nchini.
Jumapili, Septemba 11, mwaka huu,
Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kagera ili kuwapa pole waathirika wa
tetemeko hilo pamoja na kujionea madhara yaliyojitokeza.
Pia aliongoza maelfu ya wananchi
wa Manispaa ya Bukoba kuaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na
tetemeko hilo. Aliwaomba wananchi wawe watulivu na kuwaahidi kuwa
Serikali itakuwa pamoja nao.
Jumanne, Septemba 13 mwaka huu
Waziri Mkuu aliongoza hharambee ya kuchangia waathirika wa teteme hilo
na kupokea zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje
nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania.
Mbali na kusababisha vifo, watu
wengine 253 walijeruhiwa na maelfu ya wananchi walikosa makazi baada ya
nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44
ya taasisi mbalimbali za umma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
- L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, SEPTEMBA 16, 2016
EmoticonEmoticon