Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amempongeza Alexander Ceferin kuchaguliwa kuwa Rais
Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Ulaya (UEFA) katika
uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Athens nchini Ugiriki Jumatano Septemba
14, 2014.
Katika salamu zake, Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa
Ceferin ambaye ni Rais wa Chama cha Soka Slovakia ni kilelelezo cha
familia ya mpira wa miguu ya Ulaya kuona umuhimu wake katika kutumikia
shirikishi hilo sambamba na kuwa kiongozi wa FA ya Slovekia.
Rais Malinzi amesema ana imani na Ceferin kuwa ataweza kutumikia vema
nafasi zote. Malinzi ana imani Caferin ataunganisha nguvu kwa maendeleo
ya soka kwa kushirikiana na Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika
(CAF), Issa Hayatou.
Ceferin amechaguliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Michel
Platini ambaye alifungiwa na FIFA kwa miaka minane Baada ya kukutwa na
kosa la kupokea rushwa ya Pauni 1.3mil.
Rais huyu mpya alimshinda Michael Van Praag Rais wa chama cha mpira
cha Uholanzi katika kura zilizopigwa huko Athens. Ceferin atashika kiti
hicho cha uraisi mpaka mwaka 2019.
EmoticonEmoticon