Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2016/2017
inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 17, 2016 kwa michezo sita
ambayo itazikutanisha timu pinzani 12 katika viwanja sita tofauti.
Michezo ya kesho ni Mwadui FC itakayoikaribisha Young Africans kwenye
Uwanja wa CCM Kambarage. Mwadui ambayo inaingia uwanjani ikiwa na
kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stand United wakati
Young Africans ina makali ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 3-0.
Mechi nyingine yenye mvuto ni kati ya Tanzania Prisons kuwa mgeni wa
Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Azam ambayo
inaongoza ligi sawa Simba kwa kuwa zina pointi sawa, zitakutana kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Timu za Simba na Azam zina pointi 10
kila moja baada ya kucheza mechi nne ambako kila moja imeshinda mechi
tatu na kutoka sare mmoja.
Mtibwa Sugar na Kagera Sugar zinatarajiwa kukutana kwenye Uwanja wa
Manungu kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu. Mtibwa ambayo imetoka
kulazwa na Simba Jumapili iliyopita, Kagera inakwenda ugenini Morogoro
ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare tasa na Ndanda ambayo pia kesho
itakuwa ugenini kucheza na Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji.
Katika mchezo mwingine wa kesho, Ruvu Shgooting itakuwa mwenyeji wa
Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani
wakati Keshokutwa Stand United ya Shinyanga itakuwa mwenyeji wa JKT
Ruvu kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
Mzunguko wa tano wa ligi hiyo utafungwa kwa mchezo kati ya African
Lyon ya Dar es Salaam dhidi ya Toto African ya Mwanza kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam Jumanne Septemba 20, 2016. African Lyon inaingian
uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuilaza Mbao FC mabao 3-1 kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon