Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo mitano ya Mzunguko wa Nne.
Miongoni mwa michezo hiyo, itakuwa ni ile ya upinzani wa jadi kati ya
JKT Ruvu itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini
ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Stand
United kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Mbali ya michezo hiyo, pia Young Africans itakuwa mwenyeji wa
Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wakati Azam FC
ambayo itakuwa mgeni tena kwenye Uwanja wa Sokoine ikicheza na Mbeya
City na kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Ndanda itaikaribisha Kagera
Sugar ya Kagera.
Ligi hiyo
itaendelea Jumapili Septemba 11, 2016 kwa Simba kuikaribisha Mtibwa
Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, lakini uliokuwa
uzikutanishe timu za African Lyon na Mbao hapo kesho umesogezwa mbele
hadi Jumatatu Septemba 12, 2016. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Uhuru
baada ya African Lyon kubadili uwanja kutoka Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume.