Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo. |
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada ya mazungumzo yao. |
Mkuu wa mkoa wa
Arusha,Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha kwa
viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi
baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Mchungaji Solomon Masangwa , Askofu wa Kanisa la
Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na
Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro.
Katika mazungumzo na
viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira
ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo
nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya
Mungu.
Alisema kutokana na
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini
kupitia mapato ya ndani halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye
mapato hayo kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana
wajasiriamali zitakazowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji
mali.
Amewataka wawajulishe waumini wa dini zote na serikali
iko tayari kupanga utaratibu wa maafisa
maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa
elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe
inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.
Askofu Stanley Hotay
aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya
ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na
changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha alishauri kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri
wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi
uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya
kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh. Gambo amewahakikishia
viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali
inayokusudia kuitekeleza ili watoe mawazo yao katika kuiboresha na kuifanya
itekelezeke kwa wepesi zaidi.
EmoticonEmoticon