Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia), akirejesha kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo katika ofisi za CCM hii leo.
Na BMG
Nzwalile ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe Baraza Kuu Chadema Taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Chadema Mkoa wa Mwanza, amefikia uamuzi huo baada ya jana kujivua vyeo hivyo.
Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na kwamba Chadema imepoteza mwelekeo kwani kimekuwa kikiibuka na oparesheni za kuichonganisha serikali na wananchi huku pia demokrasia ikikosekana ndani ya chama hicho.
"Kama ni udikiteta basi mimi niseme Chadema ndiko kuna udikiteta kwani zaidi ya mara tatu nimemsikia Lowasa (Edward Lowasa, aliyekuwa mgombea urais 2015) akisema yeye ndiye mgombea urais mwaka 2020, kwa kikao gani". Amesema Nzwalile na kuongeza kwamba yale mambo yote mabaya yaliyokuwa yakifanyika ndani ya CCM yamenyooshwa hivyo hakuna haja ya yeye kuendelea kukaa Chadema.
Amesema atazunguka Wilaya zote ili kuhakikisha anawarejesha wengine ndani ya CCM huku akiwa na jukumu moja la kuubomoa Ukuta unaoelezwa kujengwa na Chadema kwani ni ukuta wa tope hivyo atatumia tu maji kuubomoa.
Nzwalile amekaribishwa ndani ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo, ambaye pia amewakaribisha makada wengine wa upinzani kuhamia CCM akisema kwamba chama hicho kinaendesha mambo yake kidemokrasia.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akipokea kadi ya Chadema ya aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (katikati).
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia).
Soma HAPA Taarifa ya awali.
EmoticonEmoticon