Na
Mathias Canal, Singida
Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Mkoa wa
Singida wamekabidhiwa jumla ya madawati 90 kwa kila Halmashauri ili kuondoa
adha waliyokuwa wanakumbana nayo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli alipowaagiza wakuu wa mikoa yote nchini wakati
akiwaapisha Ikulu, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.
Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka
madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya
kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa
chini wakiwa darasani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa
makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na
Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali
ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba
na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
Mtigumwe
amesema
kuwa Hali ya Madawati katika Mkoa
ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na
wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500
hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo
hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika
Halmashauri za Singida na Manyoni.
Alisema kuwa mwanzoni
mwa mwezi June mwaka huu aliteua kamati ndogo ya uratibu wa madawati kwa
kushirikisha wadau mbalimbali katika Mkoa baada ya kuona juhudi za serikali
kupitia mamlaka za Halmashauri yaManispaa na Wilaya.
Ameeleza kuwa kamati
hiyo iliweza kukusanya Jumla ya shilingi milioni 42,626,500/= kutoka kwa wadau
67 (Pesa taslimu ikiwa ni 29,046,500) wadau watano walitoa madawato 60 yenye
thamani ya shilingi 3,580,000/= na madawati 100 kutoka bonite Bottles Ltd yenye
thamaniya shilingi 10,000,000/= ambapo jumla ya madawati yaliyotengenezwa
ilikuwa ni 470.
Akisoma Taarifa ya
utengenezaji wa madawati Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Afisa Mifugo wa
mkoa wa Singida Elias Donaty Seng’ongo amesema
kuwa kupitia kamati ya kuratibu madawati walishirikisha wadau mbalimbali ikiwa
ni pamoja na Taasisi za serikali (TBA,Gispa, Tanroads, Sido, Veta, Temesa,
Sekretarieti ya Mkoa (RS), Takukuru na TRA, Mashirika ya huduma (NHC, Tanesco,
Suwasa, Posta, Taasisi za fedha (NMB, na CRDB), Mifuko ya hifadhi ya jamii
(NHIF, NSSF, na PSPF), Mashirika yasiyo ya serikali (NGO’s, SEMA, HAPA,
TUNAJALI, na HELVETAS).
Amewataja wadau wengine
waliochangia kuwa ni Vyuo vya idara za serikali (NAO, Madini, Hazina Ndogo,
Chuo cha Uhasibu, TIA, Utumishi wa Umma, Chuo cha walimu Singida, Abet English
Medium School, Maasai English medium School,
Lake School, Viwanda vya usagishaji mafuta (Mount Meru na Umoja wa wakamuaji
mafuta Mkoa wa Singida, Wafanyabiasharambalimbali, wauzaji wa vinywaji baridi)
Bonite Bottles Ltd, Wauzaji wa vipuri vya magari, Makandarasi, Wakala wa huduma
za misitu TFSAmaduka ya vifaa vya ujenzi, Hoteli na Baba na Mama Lishe Mkoani
humo.
Seng’ongo
alisema kuwa kupitia taarifa kutoka Ofisi ya Elimu
Mkoa uliweza kufikia lengo la utengenezaji wa madawati kwa asilimia 98% ambapo
juhudi bado zinaendelea kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakuwa endelevu kwa siku
zijazo.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka akitoa neno la
shukrani kwa niaba ya Wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa wa Singida
amewashukuru wadau wote waliochangia fedha Taslimu ama Madawati yakiwa tayari
yametengenezwa huku akiwasihi wadau wote kuendelee kujitolea katika kuchangia
shughuli za maendeleo katika Mkoa huo.
Pia amesema kuwa
madwati hayo ana imani yatatunzwa vizuri ili wanafunzi waweze kusoma vizuri
wakiwa wamekaa kwenye madawati kwani mwanafunzi akiketi kwenye dawati hata
mwandiko na ufahamu wake unakuwa mzuri tofauti na mwanafunzi ambaye atasoma
akiwa amekaa sakafuni hivyo kupitia upatikanaji wa madawati hayo ana imani
kubwa kuwa mkoa wa singida utaimarika kielimu na kuimarisha ufaulu wa
wanafunzi.
Naye Mfanyabiashara,
Mkulima na Mfugaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya
ya Ikungi Hassan Tati akizungumza
kwa niaba ya wadau wote waliochangia amesema kuwa Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amebuni
njia nzuri ya kuwapa motisha kwa kutoa Hati kwa wadau wote waliochangia jambo
ambalo litaamsha ari zaidi katika kuchangia shughuli za Maendeleo ya Mkoa na
taifakwa ujumla.
Tati alisema kuwa anasikitika sana pale anaposikia
kuwa mkoa wa Singida unashika nafasi ya Tano kwa umasikini katika Mikoa yote
nchini ilihali ni mkoa wenye rutuba ya kutosha na eneo pana katika uwekezaji
hivyo amewasihi wananchi na wadau kwa pamoja kushirikiana kwa pamoja katika
kukomesha umasikini huo.
EmoticonEmoticon