Viongozi
wa Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wakiteta jambo leo kwenye
Uwanja wa Kaitaba kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi
karibuni. Na sasa ukiwa tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange
ya Ligi Kuu Vodacom. Kagera Sugar wanajifua kujiandaa kwa Mchezo wao wa
tarehe 3 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui kutoka Shinyanga ambapo nmchezo
huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa tayari kwa Viwango vya
Fifa. ‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa
kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa
wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia
wamefanya usajili wakiwemo makipa. Leo wameanza kujifua kwenye Uwanja
wao kwa ajili ya kuhakikisha hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu
uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina
yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.
Wakiomba kabla ya kufanya Mazoezi leo hii jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Mwenyekiti
wa kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama ambaye pia ni Katibu wa
KRFA (katikati) kulia ni Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
(TFF), WALLACE KARIA nao walikuwepo Uwanjani hapo kujionea Uwanja huo
ambao umemalizika kwa kusuasua.
Mecky
Meximeakitoa maelekezo kwa wachezaji wake leo hii kwenye Uwanja wa
Kaitaba, Wakijiandaa kuikaribisha Timu ya Mwadui hivi karibuni.
Kwa Makini Wachezaji wa Kagera Sugar wakisikiliza Viongozi wao
Wachezaji wa Kagera Suga wakijifua leo hii hioni kwenye Uwanja wa Kaitaba
Dokta wa Timu ya Kagera Sugar(kulia) akiteta jambo na Mwamed (kushoto)
Walinda mlango wa Kagera Sugar wakijifua Vikali leo hii
Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangaru
Mashabiki
wamejitokeza kwa Wingi kuwakaribisha Kagera Sugar ambao walichezea
Misimu miwili nje ya Uwanja wa Kaitaba. Msimu ulopita Kagera waliwapa
presha kubwa wapenzi wao hadi dakika za mwisho ambapo walikuwa
wanapigania kutoshuka daraja.
Mashabiki wakiwacheki Kagera Sugar leo wakati wa Mazoezi Kaitaba
Mashabiki wa Kagera Sugar leo wamejitokeza kwa wingi kuwaona wenzao 'Wanankurukumbi' wakati wa mazoezi
Mashabiki
na Wapenzi mbalimbali wa timu ya Kagera Sugar wamejitokeza kwa Wingi
hii leo kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kupita kwa ujenzi wa
uwanja huo.
Mazoezi makali kujiandaa na Mzunguko wa Tatu wa Ligi kuu Vodacom
Makipa
wa Kagera Sugar wakijiuliza jambo leo wakati wa mazoezi yao kwa mara ya
kwanza tangu Uwanja huo umalizike kujengwa hivi karibuni. Kagera Sugar
wanajiandaa na Mchezo wao wa Ligi kuu Vodaom tarehe 3.
Mapumziko, Wachezaji wa Kagera Sugar wakipata maji ya kunywa.Kocha Mkuu wa Kagera Mecky Mexime
Shabiki wa Kagera Sugar
Straika wa Bukoba Veteran Salum Bonge nae alikuwepo Uwanjani hapo
EmoticonEmoticon