Mwakilishi
Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama akitoa salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa kongamano hilo
(hawapo pichani).
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida
akizungumzia malengo ya Kongamano la Kilimo Biashara kabla ya Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) kufungua rasmi.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akitoa hotuba ya kufungua Kongamano la
Kilimo Biashara kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa lililofanyika mwishoni mwa
wiki katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk. Charles Mahika akielezea
mikakati iliyowekwa na wizara ya kuhakikisha sekta ya kilimo, uvuvi na
mifugo inafanikiwa.
Mwezeshaji
ambaye pia ni Rais wa vijana wajasiriamali na wataalamu wa miradi ya
maendeleo mkoa wa Singida, Philemon Kiemi akitoa mafunzo ya ufugaji kuku
wa kisasa kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika
mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Mratibu wa Kongamano kutoka ESRF, Abdallah Hassan akizungumza jambo kwenye kongamano hilo.
Mwezeshaji
Bi. Kalega akitoa mafunzo ya ufugaji Kuku na matumizi ya Azolla kwa
washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa
juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Baadi
ya wakazi wa Kanda ya Ziwa akiwemo mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bi.
Mongella waliohudhuria Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika katika
ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Na Mwandishi wetu
Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, limesema litaendela kuinua fursa
za kiuchumi zinazopatikana hapa nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa
zinazoendelea kuibuliwa.
Kauli
hiyo imetolewa na Programme Specilist- Inclusive Growth UNDP Tanzania,
Ernest Salla wakati wa Kongamano la Kilimo Biashara kanda ya ziwa
lilofanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall Agosti 27 mwaka huu Jijini
Mwanza.
Kongamano
hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
kwa kushirikiana na UNDP/UNEP lililolenga kuzitambulisha fursa katika
kilimo biashara, lilihudhuriwa na wananchi mbalimbali zaidi ya 750
kutoka mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza wenyewe.
Katika
kongamano hilo Salla alisema kilimo kina fursa nyingi hivyo watanzania
hawana budi kuzitumia fursa hizo kwa kuwakumbatia wataalamu ili kiwe
mkombozi wa maisha yao.
Akizungumza
katika Kongamano hilo la siku moja, Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida
alisema licha ya uchumi wa taifa kutegemea kwa kiasi kikubwa kilimo,
lakini kilimo hapa nchini bado kipo nyuma hivyo kuchangia kiasi kidogo
katika kumuendeleza mkulima.
“Kwa
kutambua upungufu huu, ESRF ikishirkiana na UNDP/UNEP imekuwa ikifanya
tafiti mbalimbali ili kusaidia wananchi na taifa kwa ujumla kujikwamua
katika vizingiti mbalimbali vya maendeleo ukiwemo umasikini wa kipato,”
alisema Dk Kida
Alisema
kukua kwa teknolojia duniani, kumeongeza fursa nyigi za kimaendeleo
ikiwamo kilimo, kwani wakulima wengi hivi sasa hawategemei mvua na
hutumia eneo dogo kwa ajili ya kilimo.
Katika
warsha hiyo zilitolewa mada mbalimbali; pamoja na kilimo cha Foda
(Hydroponic fodder), kilimo cha mbogamboga (Hydroponic and Aquaponic
Vegetables), shamba kitalu (Green house), Azolla na ufugaji wa samaki
na nyuki kutoka kwa wakufunzi mbalimbali waliotoa ufafanuzi kuhusu fursa
mpya za kilimo biashara.
Alisema
kilimo cha kisasa au “smart farming” ambacho hakihitaji maeneo makubwa
kinaweza kufanyika katika maeneo ya mjini tofauti na izaniwavyo kuwa
kilimo lazima kiwe vijijini.
Alisema
ESRF imeshiriki katika utekelezaji wa miradi ya majaribio inayotegemea
teknolojia ya kisasa katika wilaya za Bunda, Bukoba vijijini,
Sengerema, Nyasa, Ikungi na Ileje kupitia miradi ya PEI na CDRBM kwa
kipindi cha miaka mitatu.
Pamoja
na mambo mengine, alisema matokeo ya miradi hiyo ya majaribio
yamethibitisha fursa katika kilimo biashara yanayoweza kuwasadia
wananchi katika kujikwamua na ndio miongoni mwa sababu ya kuandaa warsha
hiyo.
Akifungua
kongamno hilo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella alisema kilimo pekee ndicho chenye fursa pekee rahisi kuliko
sekta nyingine duniani kote.
Mongela
aliipongeza ESRF, UNDP, na wadau wengine wa maendeleo, kwa tafiti hizo
na kwamba hatua hiyo itasaidia kuinua uchumi wa watanzania na taifa kwa
ujumla.
Licha
ya Mongella kupongeza hatua hizo, lakini alizitaka taasisi mbalimbali
kupitia wataalamu wake kuonyesha gharama halisi za kutekeleza miradi
hiyo.
“Hizi
tekonolojia ni rahisi, watu wakianza nazo kidogokidogo baadaye watapanda
na kufika juu, tatizo la wataalamu wanasema gharama ni kubwa za
teknolojia, hivyo kuwaogopesha watu,” alisema Mongella
Amoni
Manyama kutoka UNDP, alisema kuzingatia maelekezo ya wataaalamu ndio
njia pekee ya kufanikisha katika kubuni fursa za kilimo na biashara.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk Charles Mahika alisema
wizara yake ikishirikiana nan chi zinazozunguka Ziwa Victoria wanaandaa
mwongozo wa kuanzisha ufugaji wa samaki katika vizimba na kwamba
mwongozo huo unatarajiwa kukamilishwa jijini Mwanza hivi karibuni.
Katika
kongamano hilo wapo baadhi ya wananchi waliotoa shuhuda mbalimbali
walionza kunufaika na fursa za kilimo biashara chini ya ufadhili wa UNDP
ikishirikiana na ESRF.
EmoticonEmoticon