Kocha Mkuu wa timu ya
Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya
mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31,
2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya
taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.
Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa
kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi
ambaye amefiwa na baba yake mzazi katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa
kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini
utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G
ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo
iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni:
Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC
Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
EmoticonEmoticon