Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akitoa tamko la kufungia vituo
viwili vya redio ambavyo ni Kituo cha Redio Five Arusha na Magic FM
Dar es Salaam kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam, kutokana na kukiuka Kanuni za Sheria ya Utangazaji ya mwaka
2005 kwa kurusha hewani vipindi vyenye maudhui ya uchozezi,na Kushoto ni
Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo vya Habari Bw. Jamal Zuberi wa
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Baadhi ya waandishi wa Habari
wakifuatilia tamko alilokuwa akitoa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) la kufungiwa kwa Redio
Five Arusha na Redio Magic FM Dar es Salaam leo Agosti 29,2016 Jijini
Dar es Salaam.
………………………………………………………………….
Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam.
Serikali yafungia vituo viwili vya
redio nchini kutokana na kurusha hewani taarifa za kichochezi
zinazoweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Tamko la kufungwa kwa vituo hivyo
vya redio limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,
Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari.
Aidha,Waziri Nape alivitaja vituo
hivyo kuwa ni Kituo cha Redio Five cha Arusha na Kituo cha Redio Magic
FM Dar es Salaam na alisisitiza kuwa utekelezaji wa tamko hilo unaanza
leo tarehe Agosti 29, 2016 mara baada ya kutangazwa.
“Uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo
umefikia baada ya kujiridhisha kuwa kipindi cha MATUKIO kilichorushwa
tarehe 25 Agosti ,2016 muda wa 02:00 usiku hadi 03:00 usiku na Kituo
cha Utangazaji cha Redio Five Arusha na kipindi cha cha Morning Magic
katika kipengele cha KUPAKA RANGI kilichorushwa tarehe 17 Agosti, 2016
kati ya saa 01:00 asubuhi na saa 02:00 asubuhi vilikuwa na maudhui ya
uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa amani na hivyo kukiuka masharti ya
kanuni ya 5 (a),(b),(c) na (d) pamoja na Kanuni ya Huduma za Utangazaji
(Maudhui) za mwaka 2005”, alisema Waziri Nnauye.
Waziri huyo mwenye dhamana na
vyombo vya habari nchini alisema vituo hivyo vimefungiwa kwa muda
usiojulikana na ameelekeza Kamati ya Maudhui kuviita vyombo hivyo na
kuwasikiliza kwa kina zaidi na kumshauri hatua zaidi za kuchukua kwa
mujibu wa Kanuni za Utangazaji za mwaka 2005.
Pamoja na hayo Waziri Nape
alivitahadharisha vyombo mbalimbali vya habari ,kutoshawishika kuvunja
Sheria na Kanuni zinazoongoza tasnia ya Habari ili kulinda heshima ya
tasnia ya habari na kuhakikisha nchi inabaki na Amani.
Hata hivyo Sheria ya Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003 Kifungu cha 28 (1) kimempa Mamlaka
Waziri wa mwenye dhamana na masuala ya Habari kufungia vyombo vya habari
vinavyoweza kurusha hewani habari za uchochezi.
EmoticonEmoticon