Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati
ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa
ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na
Udart, Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara
hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
Wajumbe
wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina
Malembeka (kulia), akiteta jambo na Esther Mahawe ndani ya basi la
mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya
kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati
hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.
Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.
Mkuu
wa Oparesheni wa Chumba cha kuangalia mienendo ya mabasi ya udart
yakiwa barabarani, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo
mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo
unavyofanyakazi.
………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
Kamati
ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa leo asubuhi imefanya
ziara ya siku moja ya kutembelea mradi wa Udart yenye lengo la kujua
jinsi mradi huo unavyoendeshwa pamoja na kujua changamoto zake ambapo
wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wao Jasson Rweikiza ambaye ni
Mbunge wa Bukoba vijijini.
Katika
hatua nyingine ya ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha anawaondoa
wafanyabiashara katika Miundombinu ya Kampuni ya Mabasi ya mwendo wa
haraka (Udart)
Simbachawene
alitoa agizo hilo wakati akizungumza na uongozi wa Udart baada ya
kufanyika majuisho ya ziara ya kamati ya bunge ya tawala za mikoa na
serikali za mitaa kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
“Namuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwaondoa mara moja wafanyabiashara katika miundombinu ya udart” alisema Simbachawene.
Mkurugenzi
Mkuu wa Udart, David Mgwassa alisema changamoto kubwa iliyopo ni elimu
kwa wananchi kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart.
Alisema
changamoto waliyonayo ni wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu
matumizi ya miundombinu ya udart ambapo wamejipanga kuhahikisha kila
mwananchi anaipata jambo litakalosaidia kuitunza na kuendelea kupata
huduma bora.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza aliutaka uongozi wa udart kuhakikisha
wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri jijini Dar es Salaam ili
kuwapunguzia adha ya usafiri wananchi.
Kamati
hiyo ilitembea mradi wa udart katika vituo vikuu vya Kimara mwisho,
Moroco makao makuu ya Udart Jangwani, Gerezani na Kivukoni.
EmoticonEmoticon